Kutuhusu

Bwana Yesu Asifiwe

Kama Kiongozi wa juu( Mratibu )wa maono ya Jumuiya hii ya Mahali pa Amani napenda kumshukuru Mwenyenzi  Mungu kwa nafasi aliyonipa ya kuwa msimamizi wa Huduma hii.Napenda kumshukuru  Yesu Kristo kwa  kuwa kiongozi wa Huduma hii. Napenda kumshukuru  Roho Mtakatifu kuwa msaidizi wa hii huduma. Napenda kumshukuru  mke wangu( Mrs Neema ) ambaye kwangu amefanyika nguzo muhimu sana katika maisha yangu kiroho na kimwili.
Huduma hii kwanza imedhamiria kuhubiri Injili ya Kweli  na kuweka Injili ya Kweli katika fikra za Vijana ili kuunganisha maisha yao Kiroho na maisha yao Kimwili. Kuishi  kwa  Yesu Kristo hapa duniani tutatumia kuwafundisha Vijana wote  jinsi ya kuishi Kiroho na kimwili.Kama Jumuiya tutahusika na ufundishaji/Kujifunza kuhusu  nguvu za Jina la Mungu.Jumuiya yetu itafunza Vijana kufahamu umuhimu wa maisha ya Yesu Kristo katika mwili na kiroho sambamba na jinsi Roho Mtakatifu anavyo tusaidia katika uhai wetu hapa Duniani. Mtu utaweza jiuliza kwanini tumelenga vijana na sio rika lingine!!sababu ya msingi ni hii kwamba Vijana ni moja ya mzizi wa mwili na kiroho.Biblia,Vijana  wanatajwa kama rika lenye nguvu na ambalo shetani mwenyewe uliwinda ili kupandikiza uovu. Katika kuwafundisha vijana tutasimamia mambo kadha nayo ni:
a)-Katika kujifunza juu ya Jina la Mungu kama mumba wa mbingu na nchi  ni kwamba jumuia tutajifunza kuhusu Upendo wake,haki za upendo wake,wema wa Upendo wake,Hukumu za Upendo wake, ahadi zake kwa mwanadamu,Agano lake  na mwisho faida za kumcha Mungu.
b)-Katika kujifunza juu ya maisha ya Yesu Kristo ni kwamba tutafundisha/tutajifunza,jinsi yalivyo na faida kubwa kwa mwanadamu pindi unapo  yafahamu  na kuyaishi kama ilivyo elekezwa kwenye  maandiko.
c)-Kuhusu Roho Mtakatifu ,hapa tutajifunza/kufunzwa jinsi ya kusikia sauti yake,jinsi ya kuona ishara zake,na jinsi ya kuelewa uwepo wake na kusoma ishara zake. Nasisitiza kwamba Roho Mtakatifu ni hitaji la Mteule yoyote hivyo basi kwa  Kijana anaye hitaji maisha matakatifu lazima ajifunze haya yote ili kumpokea huyu Roho wa Mungu.
Soma Biblia utafahamu kwamba Yesu Kristo alikuja duniani ili kuokoa roho za wanadamu zilizopotea. Sisi kama Jumuia hatuna mipaka ya Madhehebu wala mipaka ya kiimani  kwa Vijana na tutahudumia  wote. Uongozi wa Jumuiya kwa ushirikiano na vijana kutakuwepo  mpango mkakati wa jinsi ya kufikisha tuliyo elezea hapo juu kwa Vijana wa Madhehebu yote na dini zote. Wote watakao jiunga na Jumuiya tutahakikisha wanapata kujifunza kuishi maisha ya kiroho kama Kristo Yesu alivyo tuagiza kipindi alipo kuja Ulimwenguni kutukomboa.
KAMA KIONGOZI MKUU KATIKA JUMUIYA HII NAPENDA SANA KUKUALIKA UKAWE MSHIRIKI WA HAYA MAONO  NA UFANYIKE MMOJA  KATIKA KUUJENGA MWILI WA KRISTO YESU. MILIKI YA MUNGU HAKUNA UZEE BALI  UFALME WA MUNGU KILA SIKU UNA IMARIKA HATA MILELE.

AMEN!!

0 comments :