Somo la leo 11/09/2015

Bwana Yesu Asifiwe wapendwa


Tuombe.
 Bwana Yesu tunasema asante sana kwa wiki hii nzima ambapo ulikuwa pamoja nasi tangu mwanzo mwa wiki mpaka siku hii ya Ijumaa. Ulikuwa pamoja nasi katika semina yetu yenye kichwa " Jinsi ya kushinda majaribu kiroho na kimwili". Asante kwa maneno mbalimbali yaliyohubiriwa. Pia naomba ukawe pamoja nasi kwa siku ya leo ambapo tunaenda kumalizia semina hii. Ukatupe Roho wako Mtakatifu ili Atuwezeshe kuelewa yote tunayopaswa kuyafahamu kwa Utukufu wa Jina Lako. Amen!

Neno la asubuhi ya leo linatoka ktk kitabu cha Luka 4:1-9. Nitasoma mistari minne ya Kwanza kama ifuatavyo:
Mr Atupele Mwakalinga
1-      Kisha Yesu, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akarudi kutoka Yordani akaongozwa hadi jangwani. Alikaa huko jangwani siku arobaini. 2-akijaribiwa na shetani. Siku zote hizo hakula cho chote , kwa hiyo baada ya muda huo aliona njaa.3-Shetani akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate.”4-Yesu akamjibu, “Imeandikwa katika maandiko, ‘mtu haishi kwa chakula tu.’

Neno tajwa hapo juu na sana kama utasoma mistari yote, linatuonyesha jinsi Yesu alivyoshinda majaribu. Neno linatuambia kabla ya kujaribiwa Yesu alikuwa amejaa Roho Mtakatifu, hivyo kwa maana nyingine ni kwamba Roho Mtakatifu, huongoza kushinda majaribu kama tutakuwa naye kwa wingi katika mioyo yetu.
 Pia tunajifunza kuwa kwa kila jaribu, Yesu alikuwa analishinda kwa kifungu cha neno katika Biblia, alikuwa anasema “imeandikwa....". Hivyo basi ili kushinda majaribu ni lazima neno la Mungu likae kwa wingi ndani mwetu.
 Pia Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa "kesheni msije mkaingia majaribuni"...hili pia linatukumbusha kusali mara kwa mara ili tusije kuingia majaribuni.
 Sala ya Baba Yetu Uliye mbinguni....., inasema pia..." usitutie kwenye majaribu...” Hivyo ni vyema kumwomba Mungu atuepushe na majaribu. Lakini tukumbuke pia wakati mwingine, Mungu hukubali majariibu yatupate lakini tukiendelea kumtumaini yeye atatupa mlango wa kutokea.

Naomba Bwana Yesu azidi kuwabariki Ijumaa hii ya leo, mnapokwenda kulitafakari neno hili la leo. Amina.


2 comments :

  1. Haleluya!wana wa Mungu.napenda kueka nyongeza kwenye Neno hili la Asubuhi.
    Nimebarikiwa na neno hili toka kwa Kaka Atupele na alichofunza leo jana usiku nilikuwa nakitafakari sana.Ndugu zangu wana Jumuiya,semina hii ni moja ya eneo muhimu sana sana katika maisha yetu ya kiroho,na utaitaji sana kulifahamu,eneo hili limekuwa na mgawanyiko wa pande mbili.

    1-Upande wa Majaribu yetu wanadamu kwa Mungu.
    2-Upande wa Majaribu ya Mungu kwetu.

    ~Majaribu ya Upande wa kwanza ni yale ambayo utunyima sisi haki za Msingi katika kule kuitwa Wana wa Mungu,upande huu utatuharibia kabisa kufikia yale Mungu kama Baba ametupangia katika Maisha yetu hasa maisha ya baada ya kifo.

    ~Majaribu ya Upande wa pili haya ni yale yanatupa kuimarika zaidi kiroho,yanatupa nafasi ya kuandaliwa kiimani,yanatupa kupimwa ule utayari wetu wa mapokeo ya kile tulicho kiomba kwa Mungu na mwisho yanatupa kutambuliwa kule kumcha Mungu.

    ~Ukiwa mtu makini utaweza kutambua pande hizi mbili zina angukia kwenye makundi makubwa mawili ya Majaribu;

    a} Hasara.
    b} Faida.

    ~Katika Neno la leo utaweza kuona Yesu Kristo baada ya Kujazwa Roho Mtakatifu akapelekwa kwa Shetani hapa tunaweza sema kwamba kama ni wanafunzi basi alipelekwa chumba cha Mtihani, ambapo shetan ndio mtihani na akaachwa mwenyewe bila kusimamiwa,tukisema bila kusimamiwa tunaingia kwenye nena na kuibeba taswira ya jangwa.
    Kama ni mfanyakazi basi utasema amepelekwa chumba cha interview akiwa peke yake na shetan ndio anaye mu-interview.

    ~Ndugu mwana pPt hapa nia yetu kubwa kupitia semina hii ni wewe uweze kujifunza na ukasaidike kwenye maisha yako,tumekuwa wanadamu wa kulalamika sana,tumekuwa wanadamu wa kukimbilia Ishara sana,tunasahau kwamba haya tunayaona sio Ishara,embu fikiria habari ya akina Shadraka,Meshaki na Abednego walivorushwa kwenye Tanuru la Moto tena Moto mkali kweli kweli.Kwa wale mliobahatika kutembelea viwanda vya kufua chuma mtaweza kuelewa habari za tanuru lenye moto mkali,Biblia imeandika wale waliokuwa wamepewa kazi ya kuwatupa kwenye tanuru wao waliungua na kufa maana moto haukuwa wa kawaida.Kwa wanao fahamu hii Story tunaambiwa Mfalme Nebukadreza akaona mtu mmoja zaidi.Je unafikiri kupulizwa ukaanguka ni Muujiza kuliko uwo wakina Shadraka?,Je unadhani Ishara za watumishi wa leo wanaojiita Manabii wameshafikia ata robo ya aliyofanya Nabii wa kweli tunayesoma makubwa aliyoyafanyia unabii kama Elia?????.

    ~Semina hii ni ndefu sana ila kwa muda wiki tuliopata natumaini utakuwa umedaka kitu na utajipa mazoezi ya hicho umedaka na hakika Mungu wetu si muongo ata Neno lake liache kuwa Hai.Tena imeandikwa "neno lake limethibitika"..ni kama chapati za "Azamu"..Yani wewe unaitoa kwenye Friji kisha unaipasha tayari unaila kama umeianda wewe..Ndivo neno la Mungu liko hivo.Utalitoa kwenye Biblia kisha utalitafakari na kuanza kuliishi na ukiliishi kwa Uwaminifu basi linafanyika kitu halisi,kwa maana lishaundwa na kuifadhiwa kwa ajili yako.Chapati hizo za Azamu hauwezi zila kama hujazipashwa kwenye joto flani ndivo Neno la Mungu liko hivyo kwamba huwezi lisoma tuu ukaliamini likawa tayari kutenda.Lazima ukalisome,ukaliamini,ukalitafakari na kuliishi yani kulitendea.

    ~Mpendwa mwana wa Mungu,BWANA akubariki na siku hii akakufanyie roho mpya ya hekima,akufinyange katika kweli yake akibariki cho chote utakacho kwenda kufanya leo na akufanye mashindi wa jaribu lako leo
    Amen.

    ReplyDelete