Somo la Leo


Shaloom wana wa Mungu  katika Hemani mwa Mahali pa Amani

Ni asubuhi njema napenda kumbariki  Mungu wetu kwa kunipa hii nafasi ya kusema nawe juu ya habari njema ya Injili ya kweli kupitia semina hii yenye kichwa  cha somo kisemacho
#Jinsi ya Kushinda Majaribu Kiroho/Kimwili #
 ~Tumekuwa na wahudumu kila siku na tumekuwa tukipata kujifunza mengi kwa kila mmoja alivoguswa na Roho wa Bwana.Asubuhii hii tunaendelea na semina yetu,na leo nataka tukajifunze jinsi mwanadamu anpo fikia kumjaribu Mungu.Maana hatujifunzi sisi tu kama wanadamu kushinda majaribu lakini pia sisi kama wanadamu kushinda majaribu kwa kumjaribu Mungu.Utaweza jiuliza inakuwaje mimi kumjaribu Mungu lakini fahamu Yesu Kristo alimwambia Shetani  imeandikwa’’usimjaribu Bwana Mungu wako’’hii ikidhirisha ata sisi wanadamu tunamjaribu mara nyingi Bwana Mungu wetu.Tutaenda kusoma Neno la leo na tutalipata katika Kitabu cha KUTOKA,
**Kutoka17:2 kwa hiyo hao watu wakateta na Musa,wakasema,Tupe maji tunywe.Musa akawaambia,kwani kuteta na mimi?Mbona mnamjaribu BWANA?
~Yesu Kristo wakati wote alikuwa anafikiria kuhusu mtu kamili na haja zake zote-sio mwili na magonjwa yake tu,bali roho na nafasi vile vile.Kazi yake ya kufundisha,kuokoa,na kuponya zote zilikwenda pamoja.Si kitu kinachowezekana kuondoa huduma ya uponyaji kutoka katika huduma ya kuokoa.Hizo zote zilikuwa ni kwa ajili kusudi moja tu-kuwageuza watu kutoka dhambini,kumwelekea Mungu.Utaweza shangaa inakuwaje Neno linamuongelea Musa nami nina anza na habari za Yesu Kristo!Nia yangu nataka upate picha hizi mbili.Kwanza kabisa Musa alikuwa na wana wa Israel jangwani na walikuwa wakipitia magumu na magumu hayo yalikuwa juu ya wao kukombolewa toka katika utumwa wenye mateso toka Misri kisha kuponywa na mateso ya Misri.Katika kuongozwa na ukombozi wa Musa utaona utofauti na ukombozi wa Yesu Kristo kwa wanadamu.

~Ukisoma Neno utagundua kitu hapa kwamba  wana wa Israel walipatwa na kiu na nia ya Mungu kufanya yote kwao ni ili wao waanze kumtegemea yeye na siyo mwanadamu ,Mungu alitaka wakafahamu kabisa kwamba yeye ndiye Mungu wa kweli yeye awezaye yote na siyo mwanadamu.Wanadamu wengi wanapoingia kwenye mahusiano ya kimapenzi lazima kila mmoja atahitaji nafasi ya kuzihirisha penzi lake la kweli kwa mwenza wake,na  katika zoezi hili kuna wale ufikia mahali wakaelewa na kuna wale uchukulia hali hizo za kuonyeshana ukweli wa penzi walilobeba ni la kweli .Wengine hali hii kuna atakaye ichukuwa kama vile mwenza wake ni "mpenzi bwege" au "buzi flan"na uwa itamuumiza mtu anaye jitoa pale atakapofahamu unachukuliwa ndivyo sivyo,hali hii ya kujizihirisha uja kwa vile mmoja wa wenza hao ataitaji mwenza wake afahamu anapendwa na asiangalie tena wengine bali yeye tuu.
~Tukirudi kwenye neno utajifunza kuwa Musa anawaambia...mbona mnamjaribu BWANA?unafikiri ni mara ngapi katika maisha yako umemjaribu Bwana..!!Je umewezaje kushinda Jaribu hilo?.
Mara ngapi wewe kama mwanadamu umemjaribu BWANA?? na ahadi zako labda akikupa mume/mke utamtumaini na kumtukuza sana Mungu?
Mara ngapi wewe kama mwanadamu umemjaribu BWANA kumwambia ukikupa kazi utamtolea muda wako kwa mambo yake na sadaka nzuri?
Mara ngapi wewe kama mwanadamu umemjaribu BWANA? kwa kumwambia nipe gari siwezi kwenda semina,kanisan mkesha,kanisan ibada ya alfajiri na alipokupa unalitumia sivyo?
Mara ngapi wewe kama mwanadamu umemjaribu BWANA kwa kumwambia nataka extra cash ndiyo nisiibe tena kazini nab ado waiba kwa kuongeza hesabu au kupunguza hesabu ama kugushi risiti mbalimbali?
Mara ngapi wewe kama mwanadamu umemjaribu BWANA ukisema sitaki tena wanaume/wanawake hakuna mwaminifu uku ukisema Mungu alishakuumbia mke au mume mwema?
Mara ngapi wewe kama mwanadamu unamjaribu BWANA kwa kumuomba mchumba na kabla hajakujibu  akuletee unaanza kutumia rafiki zako wa kike na kiume wakupatie mchumba,umeanza kutumia fedha zako au nafasi yako kazini au uwezo wako kibiashara?.
Ndugu katika Kristo fahamu maisha yako unayopitia leo ni maisha ya wana wa Israel na usije kumjaribu BWANA kwa kuomba kitu kwa Mtu kisa amechelewa kukupa au kisa umefika mahali changamoto zimezidi,fahamu yeye atakupa kwakuwa alishasema ukimtumikia atakuwa nawe popote na kwa hali yoyote, amekuokoa ili akuongoze. Acha kulalamika kwa watu,acha kunung'unika kwa watu ukisema “hivi BWANA yu kati yetu au sivyo”,endelea kumnyenyekee na kumtii zaidi hasa kwenye wakati uwo mgumu nah ii ndio njia ya kushinda jaribu lako ulilo mjaribu Mungu.Utashinda jaribu lako kwa kumrudishia ahadi zake na sio kumrudishia uliyo wahi pitia kwa shida,taabu na mateso mengi ukimwambia hayo yalikuwa mazuri zaidi ya unayokumbana nayo.Anasema katika neno lake kwamba “shukuruni kwa kila jambo”hii ina maana kwamba changamoto,shida na tabu unazopitia ushukuru kwakuwa ukizimaliza mpendwa utaenda kupokea kitu chema sana kwenye Ayubu anakifananisha na dhahabu.Tunakushukuru kwa maana ametusikia,ametuletea changamoto,tabu na shida hizo ili tukizipitia tutapata tulichoandaliwa.Ndugu yangu yawezekana hujashika vizuri hapa,nataka ufahamu kwamba Mungu upend asana atukuzwe katika maisha yetu,hivo unapoomba kitu ndio nafasi yake ya kutukuzwa na ndio maana ukupitisha katika eneo la kuthaminisha utayari wako wa kupokea ulichoomba lakini kwake pia kikaonekana kwa wengine ili wakamtukuze.

Hivyo basi tufahamu kwamba matokeo ya changamoto,shida na tabu tunazokumbana nazo hasa pale tumeshamshirikisha Mungu tunaitaji kutambua ameshatusikia tulichoomba na tuko katika hali ya kuandaliwa kuja kupokea rasmi kile tumeomba.Barikiwa sana na Mungu ukiongezwa na Roho wa Mungu katika kulielewa vyema somo hili.Amen.

2 comments :

  1. be bless brother for the word of God.

    ReplyDelete
  2. MpP mahali hapa tutajifunza kwa speed ya kawaida kwani nia hasa yetu ni neno likuvae ili nawe upendeze ila mara nyingi wanasema hauwezi kupendeza na nguo ambayo haijakufit.

    ~Katika ukristo wako embu fanya Hema hili kama kioo chako ukajiangalie kama umependeza nasema hivyo maana utaweza kuta unaambiwa tuu na watu au unajiambia mwenyewe kwa habari ya Ukristo wako na kumbe watu hawajakuona wakagundua nguo ulizo vaa je zinakupendeza...!!!Dada Bless najua utanielewa zaidi wa wengine..Basi nimekuona umependeza.

    ~Ntaomba niongeze kwenye mstari wa 10/11...mistari hii miwili inamaana zake kila mmoja.na tukianza na mstari wa 10 hapa Ayubu anatufahamisha kile ana kihamini toka kwa Mungu wake.

    ~Wanadamu wengi wana kauli kama hizi za Ayubu ila wao wanazo kwa wanadamu wenzao.Ayubu alisema maneno haya akifahamu fika Mungu anaye mwamini anajua njia anayoiendea.na anatamka wazi kwamba hayo mateso ni ngazi ya kuelekea nafasi nyingine nzuri kimaisha akiilinganisha uzuri uwo na Dhahabu,akilingalisha thamani yake na dhahabu na pia akilinganisha kujaliwa kwako baada ya jaribu lake kama Dhahabu.

    ~Dhahabu ni moja ya madini yenye uhifadhi mkubwa sana wa thamani,kwenye Bank kubwa utakuta thamani ya fedha zako au mali utaweza kuifadhi katika mfumo wa dhahabu yani itaekwa kipande flani cha dhahabu kama mnara wa sabuni ya mche na kuifadhi.Dhahabu kwa mara chache uripotiwa kushuka thamani na ata kama fedha ya nchi itashuka thamani dhahabu itabakia na thamani,miaka inavozidi kwenda yenyewe inapanda thamani.Rangi yake tuu ni kiashirio tosha cha kitu cha thamani.

    ~Ukiona kitu chochote che rangi ya dhahabu tayari akili yako itashuka sana na hiyo rangi ata kama ni chuma au shaba au plastic imeshaekwa rangi ya dhahabu moja kwa moja thamani inaongezeka.

    ~Hivyo Ayubu anatuambia pindi unapitishwa kwenye majaribu na ukafahamu hili liko upande wa Mungu utaitaji neno hili kwamba yeye aijua njia uiendayo.Akisha kujaribu utatoka kama DHAHABU.

    ~Angalizo:mstari huu wa 11 kuna angalizo maana wanadamu usimamia mstari mmoja na kumaliza,Ayubu anaeleza zaidi hapa Mwana wa Mungu MpP kwamba ili kuvuka jaribu ambalo ukishavuka kuna faida kubwa utaipata na kuvikwa thamani kubwa ni kwamba...lazima mguu wako ukashikamane sana sio kidogo sana na hatua za Mungu...hatua za Mungu ni hatua utazipitia kwenye Jaribu uliloko,anaposema "sana"..anamaanisha kuna hadi kukatishwa tamaa.

    ~Sana inasimama kama zaidi ya......
    Ayubu anasema Njia yake nimeishika..kuishika inasimama kama kule kufahamu kila kitu na kutambua ata gizani..."kuna msemo usemwa Kipofu hapotei kwao"..hii inamaana kwamba anaifahamu sana haimpi tatizo la kuipita.

    ~Wala sikukengeuka,inamaana kule kuwa na wasiwasi kiasi cha kutumia njia za mkato au kurudi nyuma..basi Ndugu ukiitaji ushindi lazima uzishike njia za Bwana na usikengeuke.

    ReplyDelete