Neno la leo 14/09/2015

SEMINA YA WIKI MOJA YENYE KICHWA CHA SOMO''UNAHITAJI KUOMBA HADI UPOKE OMBI LAKO

Shaloom wana wa Mungu na MpP wote,Namshukuru Mungu aliye Hai kwa kutupa kuona asubuhi hii njema kabisa,Nikuombee wewe uliyeamka na kujisikia kugonjeka,kapokee uponyaji kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareti,Amen.Ndugu zangu wana pP na wakristo wote tunaingia katika semina mpya ambayo tunaenda kujifunza kuhusu ‘Unahitaji Kuomba hadi kupokea Ombi Lako".Niliguswa na kichwa hiki kwa sababu kadha wa kadha ila Moja ni, tumesahau kwamba tukienda mbele za Mungu kwa Unyenyekevu na uwaminifu tunapokea Ombi letu.
Kuna Mwalimu na muhubiri alikuwa akihubiri juu ya Kuomba akatoa mfano mmoja wa Baba na Mke wake waliokuwa wakitoka nyumbani asubuhi na wakielekea shamba,walidamka ili wawahi mvua isije kunyeshe kabla ya wao hawajaanda shamba lao.Walipofika nje Baba akaletewa picha ya Binty yake na ujumbe kuwa aombe.Pale pale akatupa kila kitu na kumrudisha mke wake ndani,Hapa nataka uanze kujifunza..’’utii’’,kisha  wakaonyesha unyenyekevu hichi cha pili nataka ujishike,wazazi hawa waliomba mpaka ile hali ikawaisha na ilipowaisha ni jioni hivyo shambani hawakuenda tena.Anafundisha ilipofika usiku,kijana wao yani mkwe akapiga simu na kusema walipata ajali mbaya sana na walikimbizwa hosp yeye akiwa ameumia kidogo ila mke ambaye ni Binty yao amelazwa ICU na wakati uwo wanaongea kwa simu Dokta anasema yuko vizuri atatolewa ICU atarudishwa Wodi.Hapa tukajifunza wameomba hadi wakapokea Ombi lao la Uzima wa Binty yao. Haleluya!!!
Mr. Nelson
 ~Tuombe~
 Mungu wetu na Baba yetu,jina lako litukuzwe,jina lako litukuzwe kwa Kaka huyu na Dada huyu anayekwenda kusoma Neno lako,tizama amekuwa akiomba bila kupokea,leo kwa kuongozwa nawe Kristo Yesu akapokee nguvu ya kupokea,Roho Mtakatifu msaidizi akamsaidie kujifunza ili awe anapokea ombi lake.kwa kuwa Ufalme ni wako,na nguvu,na utukufu,pasipo mwisho.
Amen!!
 #Somo letu leo tutajifunza kupitia Kitabu cha Waebrania11:6, imeandikwa;"Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza;kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko,na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
~Waebrania11:6 imeandikwa"Lakini pasipo Imani",tukianzia hapa wana wa Mungu tunaona neno "lakini"ambapo neno hili moja kwa moja utafahamu kwamba liko jambo kabla ndio maana Neno limeanza kwa kusema "lakini".Biblia inaandika kwamba alikuwepo Mtu aliitwa Henoko ambaye huyu alishuhudiwa akihamishwa asione mauti,na ndio katika haya ikaja kwamba yaliyofanyika kwa Henoko ata kwa Mwanadam wa leo linawezekana(hapa sasa ndio neno),"Lakini"..ilibidi liwepo.Nalo neno.."pasipo",likawepo hapa ili kukuambia kwamba ili uweze kuhamishwa usije kuona mauti kama Henoko unaambiwa inawezekana lakini lazima uwe na Imani ,ndio maana ikawepo neno "pasipo",haitaishia hapo kuwa uwe na Imani bali neno linaandika.."haiwezekani kumpendeza",utauliza kumpendeza nani?,Majibu ni kumpendeza Mungu Baba,Yesu Kristo mwokozi na Roho Mtakatifu msaidizi wetu,pia  maandiko yanamalizia kwa kusema..lakini ukishakuwa na Imani ile ya kumpendeza Mungu,Yesu Kristo na Roho wa Mungu utaitaji tena "kuamini"na utaitaji kuamini kwamba"Mungu yeye yuko"na yuko kwa ajili gan?"jibu rahisi sana ni kuwa yuko na uwapa thawabu wale wamtafutao".

 ~Wamtafutao,hapa ndiko hasa ntashikilia ila kabla ntaomba tufahamu kwamba hitaji la kwanza la kuomba hadi ukapokea ombi lako ni imani ambayo ukirudi mwanzo wa Waebrania11:1 hapo utaona Imani ikielezewa vizuri kwamba ni;kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo,ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

 ~Neno hakika ni hali ya upatikanaji au uwepo kiingereza tutasema "physical "...hakika kupo tayari..so yatarajiwayo ni hali ile ya sio palepale bali itaeza kuwa siku nyingine,masaa au dakika..at miaka na itaeza kuwa miezi vyote vinabanwa kwenye (yatarajiwayo~yatazamiwa kuwepo au kutokea ama kutendeka).Neno bayana itaeka ujumla au majumuisho au yoyote,chochote,lolote na yasiyoonekana itasimama kwa kuwa unatarajia basi hutakiona kwa macho ya mwili bali ya kiroho.Ubongo wa Mwanadamu utaunda hicho kitu,utaeka picha ya jinsi kilivo,kionekanavo ata kama hujapata mchozo.Katika maisha yetu ni mara nyingi tunasikia Mwanadamu akisema,"aah napata picha kumuona Ms Dinna kwenye gauni la Harusi".."Au utasikia nikipata kazi nami nianze maisha".vitu hivi wasemaji na wasikilizaji uanza kuviona na neno"aamini"..kwenye Biblia linaleta maana ya kuanza kuyaishi.

 ~Kuna mabinty ambao wana Vijana wa kiume kama marafiki kwa maana ya wapenzi na tiyari Binty ameanza kukaa kama Mke,tunasema hapa ameshaanza kuishi maisha anayotarajia ingawa hayaoni hapo.Tunasikia wanadamu wakiambiana."aah John akipata gari sijui hivi hana"..hapa wamesha tumaini kumuona John akiwa na gari physical ila washanza kumuona akiwa anaendesha.Utajiuliza sana kwanini nimeanza kuchambua neno moja moja katika mstari na kisha mifano mengi ila nia ni kukujengea msingi wa kufaham hayo unayoyasoma katika Maandiko yamebeba nini haswa.Mara nyingi sana wanadamu tumekuwa tukiomba vitu ambavo sisi wenyewe Imani zetu hazipo,yani hatuna Imani bali tuna Tumaini,,kwa kiingereza utasema "hope".."faith"...utaweza kutofautisha hivi una Imani maji ni uhai,...una Tumaini ukinywa maji utapata uhai..Una Imani Mke mwema anatoka kwa Mungu,,,una tumaini ukimsihi Mungu atakupa mke mwema..

 ~Sijui unashika hapo tofauti ya Imani"Faith"na Tumaini"Hope".
 ~Sasa utaweza kuomba ukiwa na Tumaini kwamba nikiomba hiki ntapewa lakini huna Imani ya kupewa hicho kitu maana lazima uwe na Imani ambayo inampendeza Mungu kukupa Ombi lako,Hauwezi kwenda tuu mbele za Mungu na tumaini alisema ukiomba ntakupa lakini hauna Imani ya kumpendeza maana hapa umeruka mstari,utaomba atakupa ila utaitaji Imani ya kumpendezeshesha.Utakuwa ushasikia mwanadamu anatumai akila chungwa atapona ila ukimuuliza linasaidia nini anasema nasikia tuu wanasema...hivyo alitakiwa ajifunze chungwa(kama maombi)..kisha vilivo ndani ya chungwa (Imani).vitakavo kusaidia sasa kutibu,ukisha jua sasa utamwambia mtu chungwa ni vitamin C,na kwa uhalisi wake virutubisho vyake vina chembe acid na vitu flan ambavo kwa vijidudu vya mafua vyenye uwezo huu vitazidiwa na hiyo Vitamin C kisha vitatoka kujizalisha au kuuwa makali ya kukula...

 ~Hivyo imani ni zaidi ya kuamini ila una amini kwa uhakika...inasema ni imani ni "hakika".”bayana"..chungwa uwakika ni Vitamin C na ina bayana(mchanganyiko uliofanya uwezo wa kuekwa katika kundi Vitamin c )..hivyo Imani yako ndio mwanzo wa kukupa kile umeomba yani utakuwa na uwakika na utakijarajia ukitumaini Mungu lazima atakupa kwa Ubayana wa uliyotenda kwake.Tunaitaji kama Wakristo tufahamu kwamba kupokea Ombi lako lazima utakuwa na uhakika nalo na mwisho utatimaini na haya yatabainishwa kabla hujayaona..Leo waumini wengi tunaishi kwa kufata mapokeo ya dini ambazo tuko nazo,ata wale walioteuliwa na kuishi katika Wokovu tunaishi kwa mapokeo ya Tuliyopokea toka kwa Watumishi.Nasema hivi kwa maana kuna watu tunaenda kanisan kwa sababu ulishazaliwa ukakuta utaratibu uwo,ata ukifika kanisani basi taratibu ni.zile zile.
-Wamtafutao,hapa utafahamu vyema mwanadamu yoyote anaye tafuta hachoki hadi apate anachotafuta sindio…na hapo ndiko hasa leo nitaekea msisitizo,hachoki kwakuwa kwanza ana Imani njia,kanuni na ukifanyacho ndicho hasa kitamfikisha kwenye kupata,na sidhan utatafuta juu juu tuu lazima utatafuta kwa undani zaidi,maarifa zaidi,kumbukumbu,na uelewa wa kutosha wa ukitafutacho na jinsi ya kukiendea kukipata.Wanadamu wengi tumekuwa watu wa kuomba kama sio watafutao hicho kitu,Naweza hapa kueka mifano michache,kijana wa kazi akiwa anataka kitu kwa boss wakelazima ata fahamu jinsi ya kukipata,hivo ataweza kuchukuwa ata wiki nzima akifanya yale yatampendezesha Bwana wake kisha atajiachia sasa na ombi lake akiwa na imani atapewa na kutumaini wakati akiwa anatimiza yale alimfanyia boss wake,Hii ata sisi tulishafanya tukiwa watoto,kuna wazazi walipendaufanye vizuri shule,kuna wale walipenda uwasikilize sana,kuna wale walipenda uwe msafi,kuna wale walipenda ujitoe pasipo kulalamika,Ooh!! Haleluya nahisi unashika.
-hivyo basi Mungu kama baba lazima wewe mwanaye utatenga muda wa kukusikia,utaitaji kumpendezesha kwa kila utafahamu Mungu atapendezwa nacho kabla hujaomba,pia utajumuisha yote hayo na kubwa bayana ya jibu la tarajiyo la ombi lako,



3 comments :

  1. ~Waebrania11:6 imeandikwa"Lakini pasipo Imani"...Tukianzia hapa wana wa Mungu tunaona neno "lakini"hivyo moja kwa moja utafahamu kwamba liko jambo kabla ndio maana Neno limeanza kwa kusema "lakini".Biblia inaandika kwamba alikuwepo Mtu aliitwa Henoko ambaye huyu alishuhudiwa akihamishwa asione mauti,na ndio katika haya ikaja kwamba yaliyofanyika kwa Henoko ata kwa Mwanadam wa leo linawezekana(hapa sasa ndio neno).."Lakini"..ilibidi liwepo.

    ~Neno.."pasipo"..likawepo hapa ili kukuambia ili ukahamishwe usije kuiona mauti kama Henoko unaambiwa lakini lazima uwe na Imani..ndio maana ikawepo neno "pasipo".haitaishia hapo kuwa uwe na Imani ila neno linaandika.."haiwezekani kumpendeza"..utauliza kumpendeza nani?..Majibu ni Mungu baba,Yesu Kristo mwokozi na Roho Mtakatifu msaidizi..na maandiko yanamalizia kwa kusema..lakini ukishakuwa na Imani ile ya kumpendeza Mungu,Yesu na Roho wa Mungu utaitaji tena "kuamini"na utautaji kuamini kwamba"Mungi yeye yuko"..na yuko kwa ajili gani"jibu ni kuwa yuko na uwapa thawabu wale wamtafutao".

    ~Wamtafutao,hapa ndiko hasa ntashikilia ila kabla ntaomba tufahamu kwamba hitaji la kwanza la kuomba hadi ukapokea ombi lako ni ~Imani~
    ~imani ukirudi Waebrania11:1 hapo utaona Imani ikielezewa vizuri kwamba ni;kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo,ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

    ~Neno hakika ni hali ya upatikanaji au uwepo kiingereza tutasema "physical "..hakika kupo tayari..so yatarajiwayo ni hali ile ya sio palepale bali itaeza kuwa siku nyingine,masaa au dakika..at miaka na itaeza kuwa miezi vyote vinabanwa kwenye (yatarajiwayo~yatazamiwa kuwepo au kutokea ama kutendeka).

    ~Neno bayana itaeka ujumla au majumuisho au yoyote,chochote,lolote na yasiyoonekana itasimama kwa kuwa unatarajia basi hutakiona kwa macho ya mwili bali ya kiroho.Ubongo wa Mwanadamu utaunda hicho kitu,utaeka picha ya jinsi kilivo,kionekanavo ata kama hujapata mchozo.

    ReplyDelete
  2. ~Katika maisha yetu ni mara nyingi tunasikia Mwanadamu akisema,"aah napata picha kumuona Ms Dinna kwenye gauni la Harusi".."au utasikia nikipata kazi nami nianze maisha"..vitu hivi wasemaji na wasikilizaji uanza kuviona na neno"aamini"..kwenye Biblia linaleta maana ya kuanza kuyaishi.

    ~Kuna mabinty ambao wana Vijana wa kiume kama marafiki kwa maana ya wapenzi na tiyari Binty ameanza kukaa kama Mke,tunasema hapa ameshaanza kuishi maisha anayotarajia ingawa hayaoni hapo.Tunasikia wanadamu wakiambiana."aah John akipata gari sijui hivi hana"..hapa wamesha tumaini kumuona John akiwa na gari physical ila washanza kumuona akiwa anaendesha...

    ~Utajiuliza sana kwanini nimeanza kuchambua neno moja moja katika mstari na kisha mifano mengi ila nia ni kukujengea msingi wa kufaham hayo unayoyasoma katika Maandiko yamebeba nini haswa

    ~Mara nyingi sana wanadamu tumekuwa tukiomba vitu ambavo sisi wenyewe Imani zetu hazipo,yani hatuna Imani bali tuna Tumaini,,kwa kiingereza utasema "hope".."faith"...utaweza kutofautisha hivi una Imani maji ni uhai,...una Tumaini ukinywa maji utapata uhai..Una Imani Mke mwema anatoka kwa Mungu,,,una tumaini ukimsihi Mungu atakupa mke mwema..

    ~Sijui unashika hapo tofauti ya Imani"Faith"na Tumaini"Hope".

    ~Sasa utaweza kuomba ukiwa na Tumaini kwamba nikiomba hiki ntapewa lakini huna Imani ya kupewa hicho kitu maana lazima uwe na Imani ambayo inampendeza Mungu kukupa Ombi lako,Hauwezi kwenda tuu mbele za Mungu na tumaini alisema ukiomba ntakupa lakini hauna Imani ya kumpendeza maana hapa umeruka mstari,utaomba atakupa ila utaitaji Imani ya kumpendezeshesha.

    ReplyDelete
  3. ~Utakuwa ushasikia mwanadamu anatumai akila chungwa atapona ila ukimuuliza linasaidia nini anasema nasikia tuu wanasema...hivyo alitakiwa ajifunze chungwa(kama maombi)..kisha vilivo ndani ya chungwa (Imani).vitakavo kusaidia sasa kutibu,ukisha jua sasa utamwambia mtu chungwa ni vitamin C,na kwa uhalisi wake virutubisho vyake vina chembe acid na vitu flan ambavo kwa vijidudu vya mafua vyenye uwezo huu vitazidiwa na hiyo Vitamin C kisha vitatoka kujizalisha au kuuwa makali ya kukula...

    ~Hivyo imani ni zaidi ya kuamini ila una amini kwa uhakika...inasema ni imani ni "hakika".."bayana"..chungwa uwakika ni Vitamin C na ina bayana(mchanganyiko uliofanya uwezo wa kuekwa katika kundi Vitamin c )..hivyo Imani yako ndio mwanzo wa kukupa kile umeomba yani utakuwa na uwakika na utakijarajia ukitumaini Mungu lazima atakupa kwa Ubayana wa uliyotenda kwake.

    ~Tunaitaji kama Wakristo tufahamu kwamba kupokea Ombi lako lazima utakuwa na uhakika nalo na mwisho utatimaini na haya yatabainishwa kabla hujayaona..Leo waumini wengi tunaishi kwa kufata mapokeo ya dini ambazo tuko nazo,ata wale walioteuliwa na kuishi katika Wokovu tunaishi kwa mapokeo ya Tuliyopokea toka kwa Watumishi..

    ~Nasema hivi kwa maana kuna watu tunaenda kanisan kwa sababu ulishazaliwa ukakuta utaratibu uwo,ata ukifika kanisani basi taratibu ni.zile zile.

    ReplyDelete