soma zaidi
Shaloom wana wa Mungu
Awali ya yote naomba
kusema kwamba ntammiss Brother George na nikuombe MpP usiache kumuombea ili
Roho Mtakatifu akampe usaidizi wa kukamilisha hiyo Task arudi Hema akija
kumshuhudia.Baada ya kusema hayo na kumuamini Mungu atasikia hilo basi tuende
kujifunza Neno la Mungu kupitia kichwa kisemacho#Unahitaji kuomba hadi upoke
ombi lako#.Ratiba leo inaonyesha MySoulMate angewalisha ila kuna jambo
limetokea basi neema ya Bwana iwe nanyi kupitia mimi muda huu.Kuna kipindi cha
utoto ilikuwa kuna muda unacheza na watoto wenzako na ghafla mwenzio anakuja na
kitu na badala ya kumuomba "directly ",unapitia vitu visivo kuwa na
mwelekeo wa kumuomba,utaruka sarakasi,unacheza ngoma,utatoa vichekesho,utataka
kumbeba basi tuu ukihisi atafurahii na kukupa alichobeba..Ghafla anakuja
mwengine na kusema"Teddy naomba ngumbiti".anampatia na
inaisha.unabakia ukitoa.
Fungua tena biblia yako iwe kwa simu au uko
nayo..tukasome Neno la tarehe ya leo alilotupa Mrs Jane akilileta kwa
Kiingereza ila sisi tutaenda kulisoma kwa kiswahili..imeandikwa ~Marko10:38
Yesu akawaambia, Hamjui mnaloliomba. Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi,
au kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi??
~Tuombe~
Baba
yetu uliye mbinguni,tunasema asante kwa kutupa muda huu wa kujifunza,shika akili
zetu,roho zetu na muda wetu,kwa pamoja vikasaidiwe na Roho Mtakatifu ili kusoma
na kuelewa neno lako kiusahihi,kwa ufalme ni wako,na nguvu,na utukufu,pasipo
mwisho.
~Neno linasema Yesu Kristo
akawaambia,unapoona kwenye biblia kuna alama hii(,).inakupa kupumzika kisha
utafakari,ujijengee picha ya kusikiliza na wewe..."Hamjui
mnaloliomba".kwa hali ya kawaida tuu mwana wa Mungu maneno haya ya Yesu
yanakupa picha kwa kuna kilichofanyika na ndio akagundua hawajuii...Neno
"Hamjui".haliwezi kuwepo mahali kama hakuna"unajua".yani
lazima haujui iwe na unajua.Kwahiyo hapa Yesu Kristo alishawaona hao wanadamu
aliokuwa anawaambia ila sasa leo unasoma wewe hivyo unaposoma ukakutana na
alama ya ( , )inakupa nafasi ya kujieka
wewe,akawambia,utaanza kuwaza vile ulikuwa unaomba,vile haupokei ombi,vile
hauombi hadi ukapokea ombi lako,nini kinakwamisha,nini kinafanya sipatagi,je
nayo pata ni matokeo sahihi ya nilicho omba!!!.Sio siri kama mfano nilio ananza
nao ni kwamba wanadamu leo tumekuwa kama watoto wa aina mbili nilioanza nao
kama mfano,utaona mtoto wa kwanza ndio wanadamu wengi wa leo tulivo,utumia muda
mwingi kufanya vitu ili Mungu avione kisha atupe,utakimbilia ishara,utakimbilia
kutoa,utakimbilia kufanya baridi na moto usieleweke.Utambeba Yesu ukiwa "fake".ukidhani
atakupa hitaji lako,Kisha atakuja mtoto wa pili ambaye anajiamini.Anajiamini
kuwa hana cha kumkosesha kupokea na aliamini ataomba na atapewa atapewa
kwakuomba kwa kweli toka moyon mwake,ata omba kwa tamaa bali kwa kuwa ana
hitaji.Basi utaitaji kujianda mbele za Mungu mpendwa kabla ya kwenda,wengi
hawana uwakika kuwa Mungu anauwezo na ukiombacho.Hivyo mtoto wa pili alifahamu
alichobeba mwenzie anauwezo nacho kumpatia.Neno linaendelea hapa
likisema.."Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi".au kubatizwa
ubatizo nibatizwao mimi??..tutaendelea baadae kidogo.Barikiwa sana
mpendwa.Ukatafakri zaidi.
soma zaidi
SEMINA YA WIKI MOJA YENYE KICHWA CHA SOMO''UNAHITAJI KUOMBA HADI UPOKE OMBI LAKO
Shaloom
wana wa Mungu na MpP wote,Namshukuru Mungu aliye Hai kwa kutupa kuona asubuhi
hii njema kabisa,Nikuombee wewe uliyeamka na kujisikia kugonjeka,kapokee
uponyaji kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareti,Amen.Ndugu zangu wana pP na
wakristo wote tunaingia katika semina mpya ambayo tunaenda kujifunza kuhusu ‘Unahitaji Kuomba hadi kupokea Ombi
Lako".Niliguswa na kichwa hiki kwa sababu kadha wa kadha ila Moja ni,
tumesahau kwamba tukienda mbele za Mungu kwa Unyenyekevu na uwaminifu tunapokea
Ombi letu.
Kuna
Mwalimu na muhubiri alikuwa akihubiri juu ya Kuomba akatoa mfano mmoja wa Baba
na Mke wake waliokuwa wakitoka nyumbani asubuhi na wakielekea shamba,walidamka
ili wawahi mvua isije kunyeshe kabla ya wao hawajaanda shamba lao.Walipofika
nje Baba akaletewa picha ya Binty yake na ujumbe kuwa aombe.Pale pale akatupa
kila kitu na kumrudisha mke wake ndani,Hapa nataka uanze
kujifunza..’’utii’’,kisha wakaonyesha
unyenyekevu hichi cha pili nataka ujishike,wazazi hawa waliomba mpaka ile hali
ikawaisha na ilipowaisha ni jioni hivyo shambani hawakuenda tena.Anafundisha
ilipofika usiku,kijana wao yani mkwe akapiga simu na kusema walipata ajali
mbaya sana na walikimbizwa hosp yeye akiwa ameumia kidogo ila mke ambaye ni
Binty yao amelazwa ICU na wakati uwo wanaongea kwa simu Dokta anasema yuko
vizuri atatolewa ICU atarudishwa Wodi.Hapa tukajifunza wameomba hadi wakapokea
Ombi lao la Uzima wa Binty yao. Haleluya!!!
![]() |
| Mr. Nelson |
~Tuombe~
Mungu wetu na Baba yetu,jina lako
litukuzwe,jina lako litukuzwe kwa Kaka huyu na Dada huyu anayekwenda kusoma
Neno lako,tizama amekuwa akiomba bila kupokea,leo kwa kuongozwa nawe Kristo
Yesu akapokee nguvu ya kupokea,Roho Mtakatifu msaidizi akamsaidie kujifunza ili
awe anapokea ombi lake.kwa kuwa Ufalme ni wako,na nguvu,na utukufu,pasipo
mwisho.
Amen!!
#Somo letu leo tutajifunza kupitia Kitabu cha
Waebrania11:6, imeandikwa;"Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza;kwa
maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko,na kwamba huwapa
thawabu wale wamtafutao.
~Waebrania11:6
imeandikwa"Lakini pasipo Imani",tukianzia hapa wana wa Mungu tunaona
neno "lakini"ambapo neno hili moja kwa moja utafahamu kwamba liko
jambo kabla ndio maana Neno limeanza kwa kusema "lakini".Biblia
inaandika kwamba alikuwepo Mtu aliitwa Henoko ambaye huyu alishuhudiwa akihamishwa
asione mauti,na ndio katika haya ikaja kwamba yaliyofanyika kwa Henoko ata kwa
Mwanadam wa leo linawezekana(hapa sasa ndio neno),"Lakini"..ilibidi
liwepo.Nalo neno.."pasipo",likawepo hapa ili kukuambia kwamba ili
uweze kuhamishwa usije kuona mauti kama Henoko unaambiwa inawezekana lakini
lazima uwe na Imani ,ndio maana ikawepo neno "pasipo",haitaishia hapo
kuwa uwe na Imani bali neno linaandika.."haiwezekani
kumpendeza",utauliza kumpendeza nani?,Majibu ni kumpendeza Mungu Baba,Yesu
Kristo mwokozi na Roho Mtakatifu msaidizi wetu,pia maandiko yanamalizia kwa kusema..lakini
ukishakuwa na Imani ile ya kumpendeza Mungu,Yesu Kristo na Roho wa Mungu
utaitaji tena "kuamini"na utaitaji kuamini kwamba"Mungu yeye
yuko"na yuko kwa ajili gan?"jibu rahisi sana ni kuwa yuko na uwapa
thawabu wale wamtafutao".
~Wamtafutao,hapa
ndiko hasa ntashikilia ila kabla ntaomba tufahamu kwamba hitaji la kwanza la
kuomba hadi ukapokea ombi lako ni imani ambayo ukirudi mwanzo wa Waebrania11:1
hapo utaona Imani ikielezewa vizuri kwamba ni;kuwa na hakika ya mambo
yatarajiwayo,ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
~Neno hakika ni hali ya upatikanaji au uwepo
kiingereza tutasema "physical "...hakika kupo tayari..so yatarajiwayo
ni hali ile ya sio palepale bali itaeza kuwa siku nyingine,masaa au dakika..at
miaka na itaeza kuwa miezi vyote vinabanwa kwenye (yatarajiwayo~yatazamiwa
kuwepo au kutokea ama kutendeka).Neno bayana itaeka ujumla au majumuisho au
yoyote,chochote,lolote na yasiyoonekana itasimama kwa kuwa unatarajia basi
hutakiona kwa macho ya mwili bali ya kiroho.Ubongo wa Mwanadamu utaunda hicho
kitu,utaeka picha ya jinsi kilivo,kionekanavo ata kama hujapata mchozo.Katika
maisha yetu ni mara nyingi tunasikia Mwanadamu akisema,"aah napata picha
kumuona Ms Dinna kwenye gauni la Harusi".."Au utasikia nikipata kazi
nami nianze maisha".vitu hivi wasemaji na wasikilizaji uanza kuviona na
neno"aamini"..kwenye Biblia linaleta maana ya kuanza kuyaishi.
~Kuna mabinty ambao wana Vijana wa kiume kama
marafiki kwa maana ya wapenzi na tiyari Binty ameanza kukaa kama Mke,tunasema
hapa ameshaanza kuishi maisha anayotarajia ingawa hayaoni hapo.Tunasikia
wanadamu wakiambiana."aah John akipata gari sijui hivi hana"..hapa
wamesha tumaini kumuona John akiwa na gari physical ila washanza kumuona akiwa anaendesha.Utajiuliza
sana kwanini nimeanza kuchambua neno moja moja katika mstari na kisha mifano
mengi ila nia ni kukujengea msingi wa kufaham hayo unayoyasoma katika Maandiko
yamebeba nini haswa.Mara nyingi sana wanadamu tumekuwa tukiomba vitu ambavo sisi
wenyewe Imani zetu hazipo,yani hatuna Imani bali tuna Tumaini,,kwa kiingereza
utasema "hope".."faith"...utaweza kutofautisha hivi una
Imani maji ni uhai,...una Tumaini ukinywa maji utapata uhai..Una Imani Mke
mwema anatoka kwa Mungu,,,una tumaini ukimsihi Mungu atakupa mke mwema..
~Sijui unashika hapo tofauti ya
Imani"Faith"na Tumaini"Hope".
~Sasa utaweza kuomba ukiwa na Tumaini kwamba
nikiomba hiki ntapewa lakini huna Imani ya kupewa hicho kitu maana lazima uwe
na Imani ambayo inampendeza Mungu kukupa Ombi lako,Hauwezi kwenda tuu mbele za
Mungu na tumaini alisema ukiomba ntakupa lakini hauna Imani ya kumpendeza maana
hapa umeruka mstari,utaomba atakupa ila utaitaji Imani ya kumpendezeshesha.Utakuwa
ushasikia mwanadamu anatumai akila chungwa atapona ila ukimuuliza linasaidia
nini anasema nasikia tuu wanasema...hivyo alitakiwa ajifunze chungwa(kama
maombi)..kisha vilivo ndani ya chungwa (Imani).vitakavo kusaidia sasa
kutibu,ukisha jua sasa utamwambia mtu chungwa ni vitamin C,na kwa uhalisi wake
virutubisho vyake vina chembe acid na vitu flan ambavo kwa vijidudu vya mafua
vyenye uwezo huu vitazidiwa na hiyo Vitamin C kisha vitatoka kujizalisha au
kuuwa makali ya kukula...
~Hivyo imani ni zaidi ya kuamini ila una amini
kwa uhakika...inasema ni imani ni "hakika".”bayana"..chungwa
uwakika ni Vitamin C na ina bayana(mchanganyiko uliofanya uwezo wa kuekwa
katika kundi Vitamin c )..hivyo Imani yako ndio mwanzo wa kukupa kile umeomba
yani utakuwa na uwakika na utakijarajia ukitumaini Mungu lazima atakupa kwa Ubayana
wa uliyotenda kwake.Tunaitaji kama Wakristo tufahamu kwamba kupokea Ombi lako
lazima utakuwa na uhakika nalo na mwisho utatimaini na haya yatabainishwa kabla
hujayaona..Leo waumini wengi tunaishi kwa kufata mapokeo ya dini ambazo tuko
nazo,ata wale walioteuliwa na kuishi katika Wokovu tunaishi kwa mapokeo ya Tuliyopokea
toka kwa Watumishi.Nasema hivi kwa maana kuna watu tunaenda kanisan kwa sababu
ulishazaliwa ukakuta utaratibu uwo,ata ukifika kanisani basi taratibu ni.zile
zile.
-Wamtafutao,hapa
utafahamu vyema mwanadamu yoyote anaye tafuta hachoki hadi apate anachotafuta
sindio…na hapo ndiko hasa leo nitaekea msisitizo,hachoki kwakuwa kwanza ana
Imani njia,kanuni na ukifanyacho ndicho hasa kitamfikisha kwenye kupata,na
sidhan utatafuta juu juu tuu lazima utatafuta kwa undani zaidi,maarifa
zaidi,kumbukumbu,na uelewa wa kutosha wa ukitafutacho na jinsi ya kukiendea
kukipata.Wanadamu wengi tumekuwa watu wa kuomba kama sio watafutao hicho
kitu,Naweza hapa kueka mifano michache,kijana wa kazi akiwa anataka kitu kwa
boss wakelazima ata fahamu jinsi ya kukipata,hivo ataweza kuchukuwa ata wiki
nzima akifanya yale yatampendezesha Bwana wake kisha atajiachia sasa na ombi
lake akiwa na imani atapewa na kutumaini wakati akiwa anatimiza yale alimfanyia
boss wake,Hii ata sisi tulishafanya tukiwa watoto,kuna wazazi walipendaufanye
vizuri shule,kuna wale walipenda uwasikilize sana,kuna wale walipenda uwe
msafi,kuna wale walipenda ujitoe pasipo kulalamika,Ooh!! Haleluya nahisi
unashika.
-hivyo
basi Mungu kama baba lazima wewe mwanaye utatenga muda wa kukusikia,utaitaji
kumpendezesha kwa kila utafahamu Mungu atapendezwa nacho kabla hujaomba,pia
utajumuisha yote hayo na kubwa bayana ya jibu la tarajiyo la ombi lako,
Nashukuru
kwa semina ya wiki hii ambayo kwa kweli inafunza SANA.Mratibu umegusa kitu
ambacho kinamgusa kila mmoja wetu kwa aina yake, "Jinsi ya kushinda
majaribu kiroho na kimwili"
MAJARIBU NI NINI?
Hili
NENO lina definition nyingi lakini inalenga zaidi ushawishi KUTENDA KINYUME NA
MAPENZI YA MUNGU. Kuna aina nyingi za majaribu lakini niyaongelea majaribu ya
aina mbili
1 MUNGU
MWENYEWE
Mwenyezi Mungu
huwa ana tujaribu , lakini Mwenyezi Mungu hatujaribu sisi kwa ajili ya
kutuumiza au kutukomoa, Mwenyezi Mungu anatujaribu ili KUTUPIMA IMANI YETU KWAKE, na ukiangalia wale wanaopata majaribu makubwa ni wale watu wenye imani kubwa kwa Mungu, Mungu hujaribu
watu wenye haki ( ZABURI 11:5 ), angalia wengi waliojaribiwa hata
zama zile, kina Ibrahim, Ayubu na hata YESU KRISTO mwenyewe.
![]() |
| Brother Johnson Mshana Katibu Mkuu pPc |
2 JARIBU
LA SHETANI
HILI LIKO TOFAUTI NA LA MUNGU, JARIBU la shetani ni kumjaribu mtu mwenye imani
kujaribu kumpotosha kwa kumpa ahadi nzuri nzuri, lakini pia HUJARIBU wale wenye imani Haba kwa
kuwapa anasa na kupenyeza usahaulifu wa kumuabudu Mungu, naamini itakuwa
umeelewa tofauti kati ya JARIBU la
kimungu na la kishetani.
Wapendwa
katika bwana, tumekuwa tukipata majaribu SANA katika maisha yetu haya, na
majaribu hayajaanza jana wala Leo, ni toka enzi na enzi kama ukisoma biblia
utaona manabii wengi tu hata watu wa kawaida wa kipindi kile
walivyojaribiwa.Hata Leo tunakutana na majaribu
na mitihani midogo kwa mikubwa, wengi wanashindwa KUKABILIANA nayo ndio maana unasikia watu wanajitoa hata UHAI wao wenyewe kwa kushindwa kuhimili
mitihani au majaribu ya maisha.
TUNAJARIBIWA ili KUPIMWA UIMARA WA IMANI YETU KWA MUNGU,
lakini pia tunajaribiwa ili KUMTAMBUA
MWENYEZI MUNGU (Daniel 2:28-29 , 1 Petro
1-12 ).Tumekuwa tukiishi maisha ya
kidunia na kumsahau Mungu, Mwenyezi Mungu pia ANATU-MISS, so ili atuvute kwake anatupatia ka JARIBU kadogo na ikifikia mahali huoni msaada wowote LAZIMA UKIMBILIE KWA MUNGU, angalia
Mungu wetu alivyo mwema, yaani hata uwe ume mfanya nini, ukimrudia anakupokea
kwa mikono miwili.Kama watoto wa Mungu, Kama wapenda KRISTO basi hatuna budi kufanya haya yafuatayo ili kushinda haya
majaribu au mitihani ya maisha inayokuja mbele yetu
1. KUAMINI.....ukishaamini kwamba kuna Mungu, anayejua
kila kitu KUHUSU wewe, kwamba NDIYE anayekulinda, toka uko tumboni
kwa mama YAKO NDIYE anayefuatilia
kila kitu chako BASI UTAWEZA PIA KUAMINI
KWAMBA HATA LIJE TATIZO GANI BASI ATAKUVUSHA.
2. KUJIAMINI..........ni lazima pia ujiamini mwenyewe ,
unaweza ukawa kabisa unaamini kwamba Mungu yupo lakini kutokana na KUTOJIAMINI kwako ikakupa woga wa
kufanya Yale unatakiwa kufanya ambalo lita kuweka karibu zaidi na Mungu.
3. KUTAFUTA MAARIFA........wote hapa tumesoma, japo hatulingani
elimu, kuna ile unakuta unakabiliwa na MTIHANI labda wa kumaliza kidato cha nne
au cha 6, huwa tulikuwa tunachukua PAST
PAPERS, mitihani iliyopita ili kutafuta mbinu mbalimbali za ufanyaji MASWALI katika kuukabili MTIHANI utakaokuja mbele, naamini hii
kila mtu kafanya.Sasa hata kwenye maisha ya kiroho haya TUNAISHI, tunatakiwa kutafuta maarifa kwa KUSOMA BIBLIA, ukisoma biblia utajua na utakuwa na mbinu za kujua
kukabiliana na matatizo au majaribu.Wapendwa,
tumekuwa wavivu SANA wa kusoma na ndio maana TUNAPIGWA SANA NA MITIHANI na tunashindwa ku-fight back sababu HATUNA MBINU, Mungu wetu aliye mwema SANA ametuwekea kila kitu wazi ni ile
tu kwamba tumekuwa wavivu, tu jiweke katika kusoma biblia ili kujua mbinu za KUKABILIANA na MAJARIBU.
Basi
Mungu wetu aliye mwema azidi kutuongoza katika roho na kweli kuweza kuyashinda
majaribu
MBARIKIWE
SANA
Hitimisho la Semina ya Jinsi ya Kushinda Majaribu Kiroho/Kimwili.
Shaloom
wana wa Mungu,napenda kushukuru Mungu kwa wakati huu ambayo tunaenda
kuhitimisha semina yetu ambayo kiukweli kama ulishiriki vyema toka mwanzo
tulipoanza siku ya Jumatatu tarehe 7th September 2015,basi nina
imani kwamba semina hii itakuwa imekutoa hatua moja kwenda nyingine kiroho.Wale
walio bahatika kuhudumu wametumia mioyo yao vyema, wakatumiwa na Roho Mtakatifu
katika kupitisha yale haswa Roho wa
Mungu alitaka tuyashike.Sitakuwa na mengi bali nitaeka msisitizo kidogo tuu
kabla ya kuhitimisha semina yetu iliyokuwa na kichwa kisemacho;#JINSI YA KUSHINDA
MAJARIBU KIMWILI NA KIROHO#Nilibahatika kusoma yote waliyo funza wahudumu na
pia changizi mbali mbali na niliguswa sana.Nilipata kuguswa na njia hizi mbili;
1-Kushika
Neno kwa ufahama,kulitafakari kwa undani zaidi na kuliishi kama linavoelekeza.
2-Kujikita
katika kulitenda Neno katika maisha yetu kimwili,yani kulifanyia kazi ya Mungu.
~Baada
ya Yesu Kristo kuwaita watu na kuanza kuwahubiria katika Galilaya,aliwaita
wavuvi hawa,Simon na ndugu yake,Andrea,kisha
akawaita Yakobo na ndugu yake,Yohana.Yesu Kristo aliwaita hawa watu ili kuwa
wanafunzi wake, ambapo walitakiwa kujifunza vyema Neno kisha waje kupewa kazi
kama mitume.Ndugu zangu katika Kristo imekuwa mara nyingi sana tunaposoma
vitabu vya watumishi mbali mbali hatuangalii maneno yenye utashi wa kiroho na
ukimbilia yale yenye utashi wa kimwili,Wanadamu leo tunasema tunamtegemea
Mungu,tunasema tunamtanguliza Mungu ila siyo kivitendo bali tunayosema yote
yanaishia hewani ,hewani kivipi!yanii kimaneno na siyo kivitendo.Nasema hivi
kwa maaana kwamba Yesu Kristo ndiye aliyewachagua watu wale;siyo wao
waliojichagua wala siyo wao waliojichagulia kazi ile.Leo kila mmoja wetu anapo
mahali pa kufanyia huduma lakini siyo wote waliokuwa radhi kumfuata Yesu kristo
ili kumruhusu yeye kutuongoza na kuwa ndiye mwenye kutuchagulia sisi;
![]() |
| Mr. & Mrs. Nelson |
-Kazi.
-Biashara.
-Vipawa.
-Ndoa#mke/mume
-Katika
kulitekeleza hili yani ukaitwa kama akina Simon na ndugu yake,Andrea ,kisha Yakobo
na ndugu yake, Yohana ,fahamu kabisa utaitajika kupimwa kwa kupewa JARIBU; na
jaribu hilo litakuwa la kiMungu kama alivosema Katibu Mkuu katika Neno alilo
tuhubiria na utapewa Jaribu ambalo ukilishinda basi litakupa uhalali wa wewe
kuwa;
-Muhudumu
wa Kweli utakaye tumiwa vyema na Roho Mtakatifu ukihudumu katika Injili ya
kweli ile ya Kristo.
-Kazi
ya kweli itakayo kupatia muda wa kumtukuza nayo Mungu,itakupa kipato,itakupa maendeleo
na itakuongeza utumishi wako katika Ufalme wa mbinguni.
-Biashara
ya kweli kimwili na kiroho,yenye faida za kuonekana zenye kumrudishia Mungu
shukrani.
-Vipawa
sahihi vyenye ushuhuda wa kweli wa kumvua Mwanadamu yule asiye amini Ukuu wa
Mungu katika Utatu Mtakatifu.
-Ndoa
yenye Amani,Faraja na Upendo ule wa tunda la roho ulionenwa katika Kitabu cha Wakorintho
na kujidhihirisha kwa Yesu Kristo pale msalabani.
-Kwenye
maisha ya sasa tumekuwa tukiishi kama
wanadamu wenye shingo ngumu sana,mara nyingi utakuta tunaenda makanisani kama
waumini lakini hatuoni ongezeko la imani zetu na hata tukitaka kuongezwa
tunashindwa tukifika kiwango au tunaanguka kwenye Interview/Mtihani ambao
tunajifunza hapa kama JARIBU,na kuishia kulalamika.Tunapokuwa chuo au tunapofanya
biashara flani,ama kazi yo yote,na ukagundua vitu hivi haviongezeki chukuwa hatua.Utaona ukianza vina ishia nusu,ukienda
ukafika haviendelei vinakufa,utavianda na vitaonyesha mwanga mara giza.hatua
hapa ni kurudi darasani ukajifunze kushinda MAJARIBU mbayo ndiyo MTAJI wa
MAFANIKIO yako.Njia zimetasha tajwa sana.KUSHIKA NENO NA KULISHI/KUOMBA BILA
KUKOMA.
-Biblia
inatufunza juu ya haya kwenye habari ya kipindi cha Yesu Kristo,katika sinagogi
moja ambalo Yesu kristo alikuwepo kumbe alikuwepo na kijana ambaye alikuwa
amepagawa na pepo mchafu.Jambo la kushangaza ni kwamba Yesu Kristo hakukemea
bali huyu pepo ndani ya huyo mtu akaanza kupiga kelele kwamba Yesu Kristo
amuachie alivyo ndani ya maisha ya huyu Kijana.Pepo hili lilifanya hivyo maana
lilishazoea kuishi na huyu Kijana na mbaya zaidi Biblia inatuambia huyu kijana
alikuwa mshirika wa siku nyingi wa hilo sinagogi na bado ibada hizo za sinagogi
hazikuweza muweka huru.
-Sikia
mtu wa Mungu unaye soma hitimisho hili nikuhubirie,tizama umekuwa mkristo siku
nyingi na una pepo;(pepo la tabia chafu kadha wa kadha zilizoonywa katika
Torati,tizama uwovu wa aina nyingi uliotajwa kama kitu cha kuepukwa bado
umekushika mfano wa pepo,shida na taabu za kutosha ulizopitia na unazopitia
zimekaa kama pepo na kuridhika,umaskini kimwili na kiroho umekukaa kama pepo,hofu
kiimani na kimtizamo imekaa nawe bila mabadiliko kama pepo,macho ya rohoni
yasiyo na uwezo mzuri wa kumuona mumeo au mkeo,ubongo wa rohoni usio na ufahamu
wa kutosha wa kutambua Baraka za Bwana,roho za visasi,vinyongo),haya kwenye
mabano ni baadhi ya mifano inayofananishwa na yule pepo iliye kuwa ndani ya kijana,kijana muhumini wa
sinagogi.
~Sikia
mwana wa Mungu leo hapa PLACE OF PEACE COMMUNITY tunakuambia kaa tayari maana
Yesu Kristo yuko hapa kukueka huru,huna haja ya kuangaika,wewe jitahidi kutulia
kwa Mungu,shika unayofunzwa hapa na jitahidi kufanyia kazi na utaona tuu hayo
yaliyofananishwa na pepo wa kijana wa sinagogi yataenda kufunguliwa.Leo kupitia
nguvu ile Yesu Kristo aliyokuwa nayo pale sinagogi,nakuambia hilo pepo halina
HAKI ya kuishi ndani yako,na Yesu kristo leo anakwenda kuviamuru
vikutoke,AMENI.
-Nikuache na ‘’home work’’Je,watu wanasikia habari za
Yesu Kristo kutoka kwetu wakati sisi tunapokwenda ofisini?biasharani?chuoni?mashuleni?mtaani?au
majumbani mwetu pindi tukitoka kwenye sehemu Injili ya Kweli yaani habari za
maisha ya Yesu Kristo,Injili ya kweli ya Ukuu wa jina la Mungu!Injili ya kweli
ya Ahadi za Mungu kwa Wanadamu! Agano la Mungu kwa wanadamu!na mahubiri hayo
unapata,Heman,Semina, au Makanisani?.#Barikiwa
sana Mwana wa Mungu uliye fanikiwa kusoma hadi mwisho na ukatunzwe na neno hili
ukisaidiwa na Roho Mtakatifu kulifanya likawe kweli yani likawe ni sehemu ya
maisha yako(LIFESTYLE).
soma zaidi
Bwana Yesu Asifiwe wapendwa
Tuombe.
Bwana Yesu tunasema asante sana kwa wiki hii
nzima ambapo ulikuwa pamoja nasi tangu mwanzo mwa wiki mpaka siku hii ya
Ijumaa. Ulikuwa pamoja nasi katika semina yetu yenye kichwa " Jinsi ya
kushinda majaribu kiroho na kimwili". Asante kwa maneno mbalimbali
yaliyohubiriwa. Pia naomba ukawe pamoja nasi kwa siku ya leo ambapo tunaenda
kumalizia semina hii. Ukatupe Roho wako Mtakatifu ili Atuwezeshe kuelewa yote
tunayopaswa kuyafahamu kwa Utukufu wa Jina Lako. Amen!
Neno
la asubuhi ya leo linatoka ktk kitabu cha Luka
4:1-9. Nitasoma mistari minne ya Kwanza kama ifuatavyo:
![]() |
| Mr Atupele Mwakalinga |
Neno
tajwa hapo juu na sana kama utasoma mistari yote, linatuonyesha jinsi Yesu
alivyoshinda majaribu. Neno linatuambia kabla ya kujaribiwa Yesu alikuwa amejaa Roho Mtakatifu, hivyo kwa maana
nyingine ni kwamba Roho Mtakatifu, huongoza kushinda majaribu kama tutakuwa naye kwa wingi katika mioyo yetu.
Pia tunajifunza kuwa kwa kila jaribu, Yesu alikuwa analishinda kwa kifungu cha neno katika
Biblia, alikuwa anasema “imeandikwa....". Hivyo basi ili kushinda majaribu ni lazima neno la Mungu likae
kwa wingi ndani mwetu.
Pia Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa
"kesheni msije mkaingia majaribuni"...hili
pia linatukumbusha kusali mara kwa mara ili tusije kuingia majaribuni.
Sala ya Baba Yetu Uliye mbinguni....., inasema
pia..." usitutie kwenye majaribu...”
Hivyo ni vyema kumwomba Mungu atuepushe na majaribu.
Lakini tukumbuke pia wakati mwingine, Mungu hukubali majariibu yatupate lakini tukiendelea kumtumaini yeye atatupa
mlango wa kutokea.
Naomba
Bwana Yesu azidi kuwabariki Ijumaa hii ya leo, mnapokwenda kulitafakari neno
hili la leo. Amina.
Subscribe to:
Comments
(
Atom
)






