Hitimisho la Semina 11/09/2015

Hitimisho la Semina ya Jinsi ya Kushinda Majaribu Kiroho/Kimwili.

Shaloom wana wa Mungu,napenda kushukuru Mungu kwa wakati huu ambayo tunaenda kuhitimisha semina yetu ambayo kiukweli kama ulishiriki vyema toka mwanzo tulipoanza siku ya Jumatatu tarehe 7th September 2015,basi nina imani kwamba semina hii itakuwa imekutoa hatua moja kwenda nyingine kiroho.Wale walio bahatika kuhudumu wametumia mioyo yao vyema, wakatumiwa na Roho Mtakatifu katika kupitisha yale haswa  Roho wa Mungu alitaka tuyashike.Sitakuwa na mengi bali nitaeka msisitizo kidogo tuu kabla ya kuhitimisha semina yetu iliyokuwa na kichwa kisemacho;#JINSI YA KUSHINDA MAJARIBU KIMWILI NA KIROHO#Nilibahatika kusoma yote waliyo funza wahudumu na pia changizi mbali mbali na niliguswa sana.Nilipata kuguswa na njia hizi mbili;
1-Kushika Neno kwa ufahama,kulitafakari kwa undani zaidi na kuliishi kama linavoelekeza.
2-Kujikita katika kulitenda Neno katika maisha yetu kimwili,yani kulifanyia kazi ya Mungu.
~Baada ya Yesu Kristo kuwaita watu na kuanza kuwahubiria katika Galilaya,aliwaita wavuvi  hawa,Simon na ndugu yake,Andrea,kisha akawaita Yakobo na ndugu yake,Yohana.Yesu Kristo aliwaita hawa watu ili kuwa wanafunzi wake, ambapo walitakiwa kujifunza vyema Neno kisha waje kupewa kazi kama mitume.Ndugu zangu katika Kristo imekuwa mara nyingi sana tunaposoma vitabu vya watumishi mbali mbali hatuangalii maneno yenye utashi wa kiroho na ukimbilia yale yenye utashi wa kimwili,Wanadamu leo tunasema tunamtegemea Mungu,tunasema tunamtanguliza Mungu ila siyo kivitendo bali tunayosema yote yanaishia hewani ,hewani kivipi!yanii kimaneno na siyo kivitendo.Nasema hivi kwa maaana kwamba Yesu Kristo ndiye aliyewachagua watu wale;siyo wao waliojichagua wala siyo wao waliojichagulia kazi ile.Leo kila mmoja wetu anapo mahali pa kufanyia huduma lakini siyo wote waliokuwa radhi kumfuata Yesu kristo ili kumruhusu yeye kutuongoza na kuwa ndiye mwenye kutuchagulia sisi;
Mr. & Mrs. Nelson
-Huduma.
-Kazi.
-Biashara.
-Vipawa.
-Ndoa#mke/mume
-Katika kulitekeleza hili yani ukaitwa kama akina Simon na ndugu yake,Andrea ,kisha Yakobo na ndugu yake, Yohana ,fahamu kabisa utaitajika kupimwa kwa kupewa JARIBU; na jaribu hilo litakuwa la kiMungu kama alivosema Katibu Mkuu katika Neno alilo tuhubiria na utapewa Jaribu ambalo ukilishinda basi litakupa uhalali wa wewe kuwa;
-Muhudumu wa Kweli utakaye tumiwa vyema na Roho Mtakatifu ukihudumu katika Injili ya kweli ile ya Kristo.
-Kazi ya kweli itakayo kupatia muda wa kumtukuza nayo Mungu,itakupa kipato,itakupa maendeleo na itakuongeza utumishi wako katika Ufalme wa mbinguni.
-Biashara ya kweli kimwili na kiroho,yenye faida za kuonekana zenye kumrudishia Mungu shukrani.
-Vipawa sahihi vyenye ushuhuda wa kweli wa kumvua Mwanadamu yule asiye amini Ukuu wa Mungu katika Utatu Mtakatifu.
-Ndoa yenye Amani,Faraja na Upendo ule wa tunda la roho ulionenwa katika Kitabu cha Wakorintho na kujidhihirisha kwa Yesu Kristo pale msalabani.
-Kwenye maisha ya sasa tumekuwa tukiishi  kama wanadamu wenye shingo ngumu sana,mara nyingi utakuta tunaenda makanisani kama waumini lakini hatuoni ongezeko la imani zetu na hata tukitaka kuongezwa tunashindwa tukifika kiwango au tunaanguka kwenye Interview/Mtihani ambao tunajifunza hapa kama JARIBU,na kuishia kulalamika.Tunapokuwa chuo au tunapofanya biashara flani,ama kazi yo yote,na ukagundua vitu hivi haviongezeki  chukuwa hatua.Utaona ukianza vina ishia nusu,ukienda ukafika haviendelei vinakufa,utavianda na vitaonyesha mwanga mara giza.hatua hapa ni kurudi darasani ukajifunze kushinda MAJARIBU mbayo ndiyo MTAJI wa MAFANIKIO yako.Njia zimetasha tajwa sana.KUSHIKA NENO NA KULISHI/KUOMBA BILA KUKOMA.
-Biblia inatufunza juu ya haya kwenye habari ya kipindi cha Yesu Kristo,katika sinagogi moja ambalo Yesu kristo alikuwepo kumbe alikuwepo na kijana ambaye alikuwa amepagawa na pepo mchafu.Jambo la kushangaza ni kwamba Yesu Kristo hakukemea bali huyu pepo ndani ya huyo mtu akaanza kupiga kelele kwamba Yesu Kristo amuachie alivyo ndani ya maisha ya huyu Kijana.Pepo hili lilifanya hivyo maana lilishazoea kuishi na huyu Kijana na mbaya zaidi Biblia inatuambia huyu kijana alikuwa mshirika wa siku nyingi wa hilo sinagogi na bado ibada hizo za sinagogi hazikuweza muweka huru.
-Sikia mtu wa Mungu unaye soma hitimisho hili nikuhubirie,tizama umekuwa mkristo siku nyingi na una pepo;(pepo la tabia chafu kadha wa kadha zilizoonywa katika Torati,tizama uwovu wa aina nyingi uliotajwa kama kitu cha kuepukwa bado umekushika mfano wa pepo,shida na taabu za kutosha ulizopitia na unazopitia zimekaa kama pepo na kuridhika,umaskini kimwili na kiroho umekukaa kama pepo,hofu kiimani na kimtizamo imekaa nawe bila mabadiliko kama pepo,macho ya rohoni yasiyo na uwezo mzuri wa kumuona mumeo au mkeo,ubongo wa rohoni usio na ufahamu wa kutosha wa kutambua Baraka za Bwana,roho za visasi,vinyongo),haya kwenye mabano ni baadhi ya mifano inayofananishwa na yule pepo  iliye kuwa ndani ya kijana,kijana muhumini wa sinagogi.
~Sikia mwana wa Mungu leo hapa PLACE OF PEACE COMMUNITY tunakuambia kaa tayari maana Yesu Kristo yuko hapa kukueka huru,huna haja ya kuangaika,wewe jitahidi kutulia kwa Mungu,shika unayofunzwa hapa na jitahidi kufanyia kazi na utaona tuu hayo yaliyofananishwa na pepo wa kijana wa sinagogi yataenda kufunguliwa.Leo kupitia nguvu ile Yesu Kristo aliyokuwa nayo pale sinagogi,nakuambia hilo pepo halina HAKI ya kuishi ndani yako,na Yesu kristo leo anakwenda kuviamuru vikutoke,AMENI.

-Nikuache na ‘’home work’’Je,watu wanasikia habari za Yesu Kristo kutoka kwetu wakati sisi tunapokwenda ofisini?biasharani?chuoni?mashuleni?mtaani?au majumbani mwetu pindi tukitoka kwenye sehemu Injili ya Kweli yaani habari za maisha ya Yesu Kristo,Injili ya kweli ya Ukuu wa jina la Mungu!Injili ya kweli ya Ahadi za Mungu kwa Wanadamu! Agano la Mungu kwa wanadamu!na mahubiri hayo unapata,Heman,Semina, au Makanisani?.#Barikiwa sana Mwana wa Mungu uliye fanikiwa kusoma hadi mwisho na ukatunzwe na neno hili ukisaidiwa na Roho Mtakatifu kulifanya likawe kweli yani likawe ni sehemu ya maisha yako(LIFESTYLE).

0 comments :