Neno la Leo 12/09/2015

Nashukuru kwa semina ya wiki hii ambayo kwa kweli inafunza SANA.Mratibu umegusa kitu ambacho kinamgusa kila mmoja wetu kwa aina yake, "Jinsi ya kushinda majaribu kiroho na kimwili"

MAJARIBU NI NINI?
Hili NENO lina definition nyingi lakini inalenga zaidi ushawishi KUTENDA KINYUME NA MAPENZI YA MUNGU. Kuna aina nyingi za majaribu lakini niyaongelea majaribu ya aina mbili
1      MUNGU MWENYEWE
 Mwenyezi Mungu huwa ana tujaribu , lakini Mwenyezi Mungu hatujaribu sisi kwa ajili ya kutuumiza au kutukomoa, Mwenyezi Mungu anatujaribu ili KUTUPIMA IMANI YETU KWAKE, na ukiangalia wale wanaopata majaribu makubwa ni wale watu wenye imani kubwa kwa Mungu, Mungu hujaribu watu wenye haki ( ZABURI  11:5 ), angalia wengi waliojaribiwa hata zama zile, kina Ibrahim, Ayubu na hata YESU KRISTO  mwenyewe.
Brother Johnson Mshana
Katibu Mkuu pPc
      JARIBU LA SHETANI
 HILI LIKO TOFAUTI NA LA MUNGU, JARIBU la shetani ni kumjaribu mtu mwenye imani kujaribu kumpotosha kwa kumpa ahadi nzuri nzuri, lakini pia HUJARIBU wale wenye imani Haba kwa kuwapa anasa na kupenyeza usahaulifu wa kumuabudu Mungu, naamini itakuwa umeelewa tofauti kati ya JARIBU la kimungu na la kishetani.
Wapendwa katika bwana, tumekuwa tukipata majaribu SANA katika maisha yetu haya, na majaribu hayajaanza jana wala Leo, ni toka enzi na enzi kama ukisoma biblia utaona manabii wengi tu hata watu wa kawaida wa kipindi kile walivyojaribiwa.Hata Leo tunakutana na majaribu na mitihani midogo kwa mikubwa, wengi wanashindwa KUKABILIANA nayo ndio maana unasikia watu wanajitoa hata UHAI wao wenyewe kwa kushindwa kuhimili mitihani au majaribu ya maisha.
TUNAJARIBIWA ili KUPIMWA UIMARA WA IMANI YETU KWA MUNGU, lakini pia  tunajaribiwa ili KUMTAMBUA MWENYEZI MUNGU (Daniel 2:28-29 , 1 Petro 1-12 ).Tumekuwa  tukiishi maisha ya kidunia na kumsahau Mungu, Mwenyezi Mungu pia ANATU-MISS, so ili atuvute kwake anatupatia ka JARIBU kadogo na ikifikia mahali huoni msaada wowote LAZIMA UKIMBILIE KWA MUNGU, angalia Mungu wetu alivyo mwema, yaani hata uwe ume mfanya nini, ukimrudia anakupokea kwa mikono miwili.Kama watoto wa Mungu, Kama wapenda KRISTO basi hatuna budi kufanya haya yafuatayo ili kushinda haya majaribu au mitihani ya maisha inayokuja mbele yetu

1. KUAMINI.....ukishaamini kwamba kuna Mungu, anayejua kila kitu KUHUSU wewe, kwamba NDIYE anayekulinda, toka uko tumboni kwa mama YAKO NDIYE anayefuatilia kila kitu chako BASI UTAWEZA PIA KUAMINI KWAMBA HATA LIJE TATIZO GANI BASI ATAKUVUSHA.
2. KUJIAMINI..........ni lazima pia ujiamini mwenyewe , unaweza ukawa kabisa unaamini kwamba Mungu yupo lakini kutokana na KUTOJIAMINI kwako ikakupa woga wa kufanya Yale unatakiwa kufanya ambalo lita kuweka karibu zaidi na Mungu.
3. KUTAFUTA MAARIFA........wote hapa tumesoma, japo hatulingani elimu, kuna ile unakuta unakabiliwa na MTIHANI labda wa kumaliza kidato cha nne au cha 6, huwa tulikuwa tunachukua PAST PAPERS, mitihani iliyopita ili kutafuta mbinu mbalimbali za ufanyaji MASWALI katika kuukabili MTIHANI utakaokuja mbele, naamini hii kila mtu kafanya.Sasa hata kwenye maisha ya kiroho haya TUNAISHI, tunatakiwa kutafuta maarifa kwa KUSOMA BIBLIA, ukisoma biblia utajua na utakuwa na mbinu za kujua kukabiliana na matatizo au majaribu.Wapendwa, tumekuwa wavivu SANA wa kusoma na ndio maana TUNAPIGWA SANA NA MITIHANI na tunashindwa ku-fight back sababu HATUNA MBINU, Mungu wetu aliye mwema SANA ametuwekea kila kitu wazi ni ile tu kwamba tumekuwa wavivu, tu jiweke katika kusoma biblia ili kujua mbinu za KUKABILIANA na MAJARIBU.

Basi Mungu wetu aliye mwema azidi kutuongoza katika roho na kweli kuweza kuyashinda majaribu
MBARIKIWE SANA


0 comments :