Shaloom wana wa Mungu
Awali ya yote naomba
kusema kwamba ntammiss Brother George na nikuombe MpP usiache kumuombea ili
Roho Mtakatifu akampe usaidizi wa kukamilisha hiyo Task arudi Hema akija
kumshuhudia.Baada ya kusema hayo na kumuamini Mungu atasikia hilo basi tuende
kujifunza Neno la Mungu kupitia kichwa kisemacho#Unahitaji kuomba hadi upoke
ombi lako#.Ratiba leo inaonyesha MySoulMate angewalisha ila kuna jambo
limetokea basi neema ya Bwana iwe nanyi kupitia mimi muda huu.Kuna kipindi cha
utoto ilikuwa kuna muda unacheza na watoto wenzako na ghafla mwenzio anakuja na
kitu na badala ya kumuomba "directly ",unapitia vitu visivo kuwa na
mwelekeo wa kumuomba,utaruka sarakasi,unacheza ngoma,utatoa vichekesho,utataka
kumbeba basi tuu ukihisi atafurahii na kukupa alichobeba..Ghafla anakuja
mwengine na kusema"Teddy naomba ngumbiti".anampatia na
inaisha.unabakia ukitoa.
Fungua tena biblia yako iwe kwa simu au uko
nayo..tukasome Neno la tarehe ya leo alilotupa Mrs Jane akilileta kwa
Kiingereza ila sisi tutaenda kulisoma kwa kiswahili..imeandikwa ~Marko10:38
Yesu akawaambia, Hamjui mnaloliomba. Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi,
au kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi??
~Tuombe~
Baba
yetu uliye mbinguni,tunasema asante kwa kutupa muda huu wa kujifunza,shika akili
zetu,roho zetu na muda wetu,kwa pamoja vikasaidiwe na Roho Mtakatifu ili kusoma
na kuelewa neno lako kiusahihi,kwa ufalme ni wako,na nguvu,na utukufu,pasipo
mwisho.
~Neno linasema Yesu Kristo
akawaambia,unapoona kwenye biblia kuna alama hii(,).inakupa kupumzika kisha
utafakari,ujijengee picha ya kusikiliza na wewe..."Hamjui
mnaloliomba".kwa hali ya kawaida tuu mwana wa Mungu maneno haya ya Yesu
yanakupa picha kwa kuna kilichofanyika na ndio akagundua hawajuii...Neno
"Hamjui".haliwezi kuwepo mahali kama hakuna"unajua".yani
lazima haujui iwe na unajua.Kwahiyo hapa Yesu Kristo alishawaona hao wanadamu
aliokuwa anawaambia ila sasa leo unasoma wewe hivyo unaposoma ukakutana na
alama ya ( , )inakupa nafasi ya kujieka
wewe,akawambia,utaanza kuwaza vile ulikuwa unaomba,vile haupokei ombi,vile
hauombi hadi ukapokea ombi lako,nini kinakwamisha,nini kinafanya sipatagi,je
nayo pata ni matokeo sahihi ya nilicho omba!!!.Sio siri kama mfano nilio ananza
nao ni kwamba wanadamu leo tumekuwa kama watoto wa aina mbili nilioanza nao
kama mfano,utaona mtoto wa kwanza ndio wanadamu wengi wa leo tulivo,utumia muda
mwingi kufanya vitu ili Mungu avione kisha atupe,utakimbilia ishara,utakimbilia
kutoa,utakimbilia kufanya baridi na moto usieleweke.Utambeba Yesu ukiwa "fake".ukidhani
atakupa hitaji lako,Kisha atakuja mtoto wa pili ambaye anajiamini.Anajiamini
kuwa hana cha kumkosesha kupokea na aliamini ataomba na atapewa atapewa
kwakuomba kwa kweli toka moyon mwake,ata omba kwa tamaa bali kwa kuwa ana
hitaji.Basi utaitaji kujianda mbele za Mungu mpendwa kabla ya kwenda,wengi
hawana uwakika kuwa Mungu anauwezo na ukiombacho.Hivyo mtoto wa pili alifahamu
alichobeba mwenzie anauwezo nacho kumpatia.Neno linaendelea hapa
likisema.."Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi".au kubatizwa
ubatizo nibatizwao mimi??..tutaendelea baadae kidogo.Barikiwa sana
mpendwa.Ukatafakri zaidi.
0 comments :