Neno la leo 16/09/2015

Shaloom wana wa Mungu

Awali ya yote naomba kusema kwamba ntammiss Brother George na nikuombe MpP usiache kumuombea ili Roho Mtakatifu akampe usaidizi wa kukamilisha hiyo Task arudi Hema akija kumshuhudia.Baada ya kusema hayo na kumuamini Mungu atasikia hilo basi tuende kujifunza Neno la Mungu kupitia kichwa kisemacho#Unahitaji kuomba hadi upoke ombi lako#.Ratiba leo inaonyesha MySoulMate angewalisha ila kuna jambo limetokea basi neema ya Bwana iwe nanyi kupitia mimi muda huu.Kuna kipindi cha utoto ilikuwa kuna muda unacheza na watoto wenzako na ghafla mwenzio anakuja na kitu na badala ya kumuomba "directly ",unapitia vitu visivo kuwa na mwelekeo wa kumuomba,utaruka sarakasi,unacheza ngoma,utatoa vichekesho,utataka kumbeba basi tuu ukihisi atafurahii na kukupa alichobeba..Ghafla anakuja mwengine na kusema"Teddy naomba ngumbiti".anampatia na inaisha.unabakia ukitoa.
Fungua tena biblia yako iwe kwa simu au uko nayo..tukasome Neno la tarehe ya leo alilotupa Mrs Jane akilileta kwa Kiingereza ila sisi tutaenda kulisoma kwa kiswahili..imeandikwa ~Marko10:38 Yesu akawaambia, Hamjui mnaloliomba. Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi, au kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi??
~Tuombe~
 Baba yetu uliye mbinguni,tunasema asante kwa kutupa muda huu wa kujifunza,shika akili zetu,roho zetu na muda wetu,kwa pamoja vikasaidiwe na Roho Mtakatifu ili kusoma na kuelewa neno lako kiusahihi,kwa ufalme ni wako,na nguvu,na utukufu,pasipo mwisho.
 Amen!!
Mr. Nelson Njau, Ath


~Neno linasema Yesu Kristo akawaambia,unapoona kwenye biblia kuna alama hii(,).inakupa kupumzika kisha utafakari,ujijengee picha ya kusikiliza na wewe..."Hamjui mnaloliomba".kwa hali ya kawaida tuu mwana wa Mungu maneno haya ya Yesu yanakupa picha kwa kuna kilichofanyika na ndio akagundua hawajuii...Neno "Hamjui".haliwezi kuwepo mahali kama hakuna"unajua".yani lazima haujui iwe na unajua.Kwahiyo hapa Yesu Kristo alishawaona hao wanadamu aliokuwa anawaambia ila sasa leo unasoma wewe hivyo unaposoma ukakutana na alama ya (  ,  )inakupa nafasi ya kujieka wewe,akawambia,utaanza kuwaza vile ulikuwa unaomba,vile haupokei ombi,vile hauombi hadi ukapokea ombi lako,nini kinakwamisha,nini kinafanya sipatagi,je nayo pata ni matokeo sahihi ya nilicho omba!!!.Sio siri kama mfano nilio ananza nao ni kwamba wanadamu leo tumekuwa kama watoto wa aina mbili nilioanza nao kama mfano,utaona mtoto wa kwanza ndio wanadamu wengi wa leo tulivo,utumia muda mwingi kufanya vitu ili Mungu avione kisha atupe,utakimbilia ishara,utakimbilia kutoa,utakimbilia kufanya baridi na moto usieleweke.Utambeba Yesu ukiwa "fake".ukidhani atakupa hitaji lako,Kisha atakuja mtoto wa pili ambaye anajiamini.Anajiamini kuwa hana cha kumkosesha kupokea na aliamini ataomba na atapewa atapewa kwakuomba kwa kweli toka moyon mwake,ata omba kwa tamaa bali kwa kuwa ana hitaji.Basi utaitaji kujianda mbele za Mungu mpendwa kabla ya kwenda,wengi hawana uwakika kuwa Mungu anauwezo na ukiombacho.Hivyo mtoto wa pili alifahamu alichobeba mwenzie anauwezo nacho kumpatia.Neno linaendelea hapa likisema.."Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi".au kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi??..tutaendelea baadae kidogo.Barikiwa sana mpendwa.Ukatafakri zaidi.

0 comments :

Neno la leo 14/09/2015

SEMINA YA WIKI MOJA YENYE KICHWA CHA SOMO''UNAHITAJI KUOMBA HADI UPOKE OMBI LAKO

Shaloom wana wa Mungu na MpP wote,Namshukuru Mungu aliye Hai kwa kutupa kuona asubuhi hii njema kabisa,Nikuombee wewe uliyeamka na kujisikia kugonjeka,kapokee uponyaji kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareti,Amen.Ndugu zangu wana pP na wakristo wote tunaingia katika semina mpya ambayo tunaenda kujifunza kuhusu ‘Unahitaji Kuomba hadi kupokea Ombi Lako".Niliguswa na kichwa hiki kwa sababu kadha wa kadha ila Moja ni, tumesahau kwamba tukienda mbele za Mungu kwa Unyenyekevu na uwaminifu tunapokea Ombi letu.
Kuna Mwalimu na muhubiri alikuwa akihubiri juu ya Kuomba akatoa mfano mmoja wa Baba na Mke wake waliokuwa wakitoka nyumbani asubuhi na wakielekea shamba,walidamka ili wawahi mvua isije kunyeshe kabla ya wao hawajaanda shamba lao.Walipofika nje Baba akaletewa picha ya Binty yake na ujumbe kuwa aombe.Pale pale akatupa kila kitu na kumrudisha mke wake ndani,Hapa nataka uanze kujifunza..’’utii’’,kisha  wakaonyesha unyenyekevu hichi cha pili nataka ujishike,wazazi hawa waliomba mpaka ile hali ikawaisha na ilipowaisha ni jioni hivyo shambani hawakuenda tena.Anafundisha ilipofika usiku,kijana wao yani mkwe akapiga simu na kusema walipata ajali mbaya sana na walikimbizwa hosp yeye akiwa ameumia kidogo ila mke ambaye ni Binty yao amelazwa ICU na wakati uwo wanaongea kwa simu Dokta anasema yuko vizuri atatolewa ICU atarudishwa Wodi.Hapa tukajifunza wameomba hadi wakapokea Ombi lao la Uzima wa Binty yao. Haleluya!!!
Mr. Nelson
 ~Tuombe~
 Mungu wetu na Baba yetu,jina lako litukuzwe,jina lako litukuzwe kwa Kaka huyu na Dada huyu anayekwenda kusoma Neno lako,tizama amekuwa akiomba bila kupokea,leo kwa kuongozwa nawe Kristo Yesu akapokee nguvu ya kupokea,Roho Mtakatifu msaidizi akamsaidie kujifunza ili awe anapokea ombi lake.kwa kuwa Ufalme ni wako,na nguvu,na utukufu,pasipo mwisho.
Amen!!
 #Somo letu leo tutajifunza kupitia Kitabu cha Waebrania11:6, imeandikwa;"Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza;kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko,na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
~Waebrania11:6 imeandikwa"Lakini pasipo Imani",tukianzia hapa wana wa Mungu tunaona neno "lakini"ambapo neno hili moja kwa moja utafahamu kwamba liko jambo kabla ndio maana Neno limeanza kwa kusema "lakini".Biblia inaandika kwamba alikuwepo Mtu aliitwa Henoko ambaye huyu alishuhudiwa akihamishwa asione mauti,na ndio katika haya ikaja kwamba yaliyofanyika kwa Henoko ata kwa Mwanadam wa leo linawezekana(hapa sasa ndio neno),"Lakini"..ilibidi liwepo.Nalo neno.."pasipo",likawepo hapa ili kukuambia kwamba ili uweze kuhamishwa usije kuona mauti kama Henoko unaambiwa inawezekana lakini lazima uwe na Imani ,ndio maana ikawepo neno "pasipo",haitaishia hapo kuwa uwe na Imani bali neno linaandika.."haiwezekani kumpendeza",utauliza kumpendeza nani?,Majibu ni kumpendeza Mungu Baba,Yesu Kristo mwokozi na Roho Mtakatifu msaidizi wetu,pia  maandiko yanamalizia kwa kusema..lakini ukishakuwa na Imani ile ya kumpendeza Mungu,Yesu Kristo na Roho wa Mungu utaitaji tena "kuamini"na utaitaji kuamini kwamba"Mungu yeye yuko"na yuko kwa ajili gan?"jibu rahisi sana ni kuwa yuko na uwapa thawabu wale wamtafutao".

 ~Wamtafutao,hapa ndiko hasa ntashikilia ila kabla ntaomba tufahamu kwamba hitaji la kwanza la kuomba hadi ukapokea ombi lako ni imani ambayo ukirudi mwanzo wa Waebrania11:1 hapo utaona Imani ikielezewa vizuri kwamba ni;kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo,ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

 ~Neno hakika ni hali ya upatikanaji au uwepo kiingereza tutasema "physical "...hakika kupo tayari..so yatarajiwayo ni hali ile ya sio palepale bali itaeza kuwa siku nyingine,masaa au dakika..at miaka na itaeza kuwa miezi vyote vinabanwa kwenye (yatarajiwayo~yatazamiwa kuwepo au kutokea ama kutendeka).Neno bayana itaeka ujumla au majumuisho au yoyote,chochote,lolote na yasiyoonekana itasimama kwa kuwa unatarajia basi hutakiona kwa macho ya mwili bali ya kiroho.Ubongo wa Mwanadamu utaunda hicho kitu,utaeka picha ya jinsi kilivo,kionekanavo ata kama hujapata mchozo.Katika maisha yetu ni mara nyingi tunasikia Mwanadamu akisema,"aah napata picha kumuona Ms Dinna kwenye gauni la Harusi".."Au utasikia nikipata kazi nami nianze maisha".vitu hivi wasemaji na wasikilizaji uanza kuviona na neno"aamini"..kwenye Biblia linaleta maana ya kuanza kuyaishi.

 ~Kuna mabinty ambao wana Vijana wa kiume kama marafiki kwa maana ya wapenzi na tiyari Binty ameanza kukaa kama Mke,tunasema hapa ameshaanza kuishi maisha anayotarajia ingawa hayaoni hapo.Tunasikia wanadamu wakiambiana."aah John akipata gari sijui hivi hana"..hapa wamesha tumaini kumuona John akiwa na gari physical ila washanza kumuona akiwa anaendesha.Utajiuliza sana kwanini nimeanza kuchambua neno moja moja katika mstari na kisha mifano mengi ila nia ni kukujengea msingi wa kufaham hayo unayoyasoma katika Maandiko yamebeba nini haswa.Mara nyingi sana wanadamu tumekuwa tukiomba vitu ambavo sisi wenyewe Imani zetu hazipo,yani hatuna Imani bali tuna Tumaini,,kwa kiingereza utasema "hope".."faith"...utaweza kutofautisha hivi una Imani maji ni uhai,...una Tumaini ukinywa maji utapata uhai..Una Imani Mke mwema anatoka kwa Mungu,,,una tumaini ukimsihi Mungu atakupa mke mwema..

 ~Sijui unashika hapo tofauti ya Imani"Faith"na Tumaini"Hope".
 ~Sasa utaweza kuomba ukiwa na Tumaini kwamba nikiomba hiki ntapewa lakini huna Imani ya kupewa hicho kitu maana lazima uwe na Imani ambayo inampendeza Mungu kukupa Ombi lako,Hauwezi kwenda tuu mbele za Mungu na tumaini alisema ukiomba ntakupa lakini hauna Imani ya kumpendeza maana hapa umeruka mstari,utaomba atakupa ila utaitaji Imani ya kumpendezeshesha.Utakuwa ushasikia mwanadamu anatumai akila chungwa atapona ila ukimuuliza linasaidia nini anasema nasikia tuu wanasema...hivyo alitakiwa ajifunze chungwa(kama maombi)..kisha vilivo ndani ya chungwa (Imani).vitakavo kusaidia sasa kutibu,ukisha jua sasa utamwambia mtu chungwa ni vitamin C,na kwa uhalisi wake virutubisho vyake vina chembe acid na vitu flan ambavo kwa vijidudu vya mafua vyenye uwezo huu vitazidiwa na hiyo Vitamin C kisha vitatoka kujizalisha au kuuwa makali ya kukula...

 ~Hivyo imani ni zaidi ya kuamini ila una amini kwa uhakika...inasema ni imani ni "hakika".”bayana"..chungwa uwakika ni Vitamin C na ina bayana(mchanganyiko uliofanya uwezo wa kuekwa katika kundi Vitamin c )..hivyo Imani yako ndio mwanzo wa kukupa kile umeomba yani utakuwa na uwakika na utakijarajia ukitumaini Mungu lazima atakupa kwa Ubayana wa uliyotenda kwake.Tunaitaji kama Wakristo tufahamu kwamba kupokea Ombi lako lazima utakuwa na uhakika nalo na mwisho utatimaini na haya yatabainishwa kabla hujayaona..Leo waumini wengi tunaishi kwa kufata mapokeo ya dini ambazo tuko nazo,ata wale walioteuliwa na kuishi katika Wokovu tunaishi kwa mapokeo ya Tuliyopokea toka kwa Watumishi.Nasema hivi kwa maana kuna watu tunaenda kanisan kwa sababu ulishazaliwa ukakuta utaratibu uwo,ata ukifika kanisani basi taratibu ni.zile zile.
-Wamtafutao,hapa utafahamu vyema mwanadamu yoyote anaye tafuta hachoki hadi apate anachotafuta sindio…na hapo ndiko hasa leo nitaekea msisitizo,hachoki kwakuwa kwanza ana Imani njia,kanuni na ukifanyacho ndicho hasa kitamfikisha kwenye kupata,na sidhan utatafuta juu juu tuu lazima utatafuta kwa undani zaidi,maarifa zaidi,kumbukumbu,na uelewa wa kutosha wa ukitafutacho na jinsi ya kukiendea kukipata.Wanadamu wengi tumekuwa watu wa kuomba kama sio watafutao hicho kitu,Naweza hapa kueka mifano michache,kijana wa kazi akiwa anataka kitu kwa boss wakelazima ata fahamu jinsi ya kukipata,hivo ataweza kuchukuwa ata wiki nzima akifanya yale yatampendezesha Bwana wake kisha atajiachia sasa na ombi lake akiwa na imani atapewa na kutumaini wakati akiwa anatimiza yale alimfanyia boss wake,Hii ata sisi tulishafanya tukiwa watoto,kuna wazazi walipendaufanye vizuri shule,kuna wale walipenda uwasikilize sana,kuna wale walipenda uwe msafi,kuna wale walipenda ujitoe pasipo kulalamika,Ooh!! Haleluya nahisi unashika.
-hivyo basi Mungu kama baba lazima wewe mwanaye utatenga muda wa kukusikia,utaitaji kumpendezesha kwa kila utafahamu Mungu atapendezwa nacho kabla hujaomba,pia utajumuisha yote hayo na kubwa bayana ya jibu la tarajiyo la ombi lako,



3 comments :

Neno la Leo 12/09/2015

Nashukuru kwa semina ya wiki hii ambayo kwa kweli inafunza SANA.Mratibu umegusa kitu ambacho kinamgusa kila mmoja wetu kwa aina yake, "Jinsi ya kushinda majaribu kiroho na kimwili"

MAJARIBU NI NINI?
Hili NENO lina definition nyingi lakini inalenga zaidi ushawishi KUTENDA KINYUME NA MAPENZI YA MUNGU. Kuna aina nyingi za majaribu lakini niyaongelea majaribu ya aina mbili
1      MUNGU MWENYEWE
 Mwenyezi Mungu huwa ana tujaribu , lakini Mwenyezi Mungu hatujaribu sisi kwa ajili ya kutuumiza au kutukomoa, Mwenyezi Mungu anatujaribu ili KUTUPIMA IMANI YETU KWAKE, na ukiangalia wale wanaopata majaribu makubwa ni wale watu wenye imani kubwa kwa Mungu, Mungu hujaribu watu wenye haki ( ZABURI  11:5 ), angalia wengi waliojaribiwa hata zama zile, kina Ibrahim, Ayubu na hata YESU KRISTO  mwenyewe.
Brother Johnson Mshana
Katibu Mkuu pPc
      JARIBU LA SHETANI
 HILI LIKO TOFAUTI NA LA MUNGU, JARIBU la shetani ni kumjaribu mtu mwenye imani kujaribu kumpotosha kwa kumpa ahadi nzuri nzuri, lakini pia HUJARIBU wale wenye imani Haba kwa kuwapa anasa na kupenyeza usahaulifu wa kumuabudu Mungu, naamini itakuwa umeelewa tofauti kati ya JARIBU la kimungu na la kishetani.
Wapendwa katika bwana, tumekuwa tukipata majaribu SANA katika maisha yetu haya, na majaribu hayajaanza jana wala Leo, ni toka enzi na enzi kama ukisoma biblia utaona manabii wengi tu hata watu wa kawaida wa kipindi kile walivyojaribiwa.Hata Leo tunakutana na majaribu na mitihani midogo kwa mikubwa, wengi wanashindwa KUKABILIANA nayo ndio maana unasikia watu wanajitoa hata UHAI wao wenyewe kwa kushindwa kuhimili mitihani au majaribu ya maisha.
TUNAJARIBIWA ili KUPIMWA UIMARA WA IMANI YETU KWA MUNGU, lakini pia  tunajaribiwa ili KUMTAMBUA MWENYEZI MUNGU (Daniel 2:28-29 , 1 Petro 1-12 ).Tumekuwa  tukiishi maisha ya kidunia na kumsahau Mungu, Mwenyezi Mungu pia ANATU-MISS, so ili atuvute kwake anatupatia ka JARIBU kadogo na ikifikia mahali huoni msaada wowote LAZIMA UKIMBILIE KWA MUNGU, angalia Mungu wetu alivyo mwema, yaani hata uwe ume mfanya nini, ukimrudia anakupokea kwa mikono miwili.Kama watoto wa Mungu, Kama wapenda KRISTO basi hatuna budi kufanya haya yafuatayo ili kushinda haya majaribu au mitihani ya maisha inayokuja mbele yetu

1. KUAMINI.....ukishaamini kwamba kuna Mungu, anayejua kila kitu KUHUSU wewe, kwamba NDIYE anayekulinda, toka uko tumboni kwa mama YAKO NDIYE anayefuatilia kila kitu chako BASI UTAWEZA PIA KUAMINI KWAMBA HATA LIJE TATIZO GANI BASI ATAKUVUSHA.
2. KUJIAMINI..........ni lazima pia ujiamini mwenyewe , unaweza ukawa kabisa unaamini kwamba Mungu yupo lakini kutokana na KUTOJIAMINI kwako ikakupa woga wa kufanya Yale unatakiwa kufanya ambalo lita kuweka karibu zaidi na Mungu.
3. KUTAFUTA MAARIFA........wote hapa tumesoma, japo hatulingani elimu, kuna ile unakuta unakabiliwa na MTIHANI labda wa kumaliza kidato cha nne au cha 6, huwa tulikuwa tunachukua PAST PAPERS, mitihani iliyopita ili kutafuta mbinu mbalimbali za ufanyaji MASWALI katika kuukabili MTIHANI utakaokuja mbele, naamini hii kila mtu kafanya.Sasa hata kwenye maisha ya kiroho haya TUNAISHI, tunatakiwa kutafuta maarifa kwa KUSOMA BIBLIA, ukisoma biblia utajua na utakuwa na mbinu za kujua kukabiliana na matatizo au majaribu.Wapendwa, tumekuwa wavivu SANA wa kusoma na ndio maana TUNAPIGWA SANA NA MITIHANI na tunashindwa ku-fight back sababu HATUNA MBINU, Mungu wetu aliye mwema SANA ametuwekea kila kitu wazi ni ile tu kwamba tumekuwa wavivu, tu jiweke katika kusoma biblia ili kujua mbinu za KUKABILIANA na MAJARIBU.

Basi Mungu wetu aliye mwema azidi kutuongoza katika roho na kweli kuweza kuyashinda majaribu
MBARIKIWE SANA


0 comments :

Hitimisho la Semina 11/09/2015

Hitimisho la Semina ya Jinsi ya Kushinda Majaribu Kiroho/Kimwili.

Shaloom wana wa Mungu,napenda kushukuru Mungu kwa wakati huu ambayo tunaenda kuhitimisha semina yetu ambayo kiukweli kama ulishiriki vyema toka mwanzo tulipoanza siku ya Jumatatu tarehe 7th September 2015,basi nina imani kwamba semina hii itakuwa imekutoa hatua moja kwenda nyingine kiroho.Wale walio bahatika kuhudumu wametumia mioyo yao vyema, wakatumiwa na Roho Mtakatifu katika kupitisha yale haswa  Roho wa Mungu alitaka tuyashike.Sitakuwa na mengi bali nitaeka msisitizo kidogo tuu kabla ya kuhitimisha semina yetu iliyokuwa na kichwa kisemacho;#JINSI YA KUSHINDA MAJARIBU KIMWILI NA KIROHO#Nilibahatika kusoma yote waliyo funza wahudumu na pia changizi mbali mbali na niliguswa sana.Nilipata kuguswa na njia hizi mbili;
1-Kushika Neno kwa ufahama,kulitafakari kwa undani zaidi na kuliishi kama linavoelekeza.
2-Kujikita katika kulitenda Neno katika maisha yetu kimwili,yani kulifanyia kazi ya Mungu.
~Baada ya Yesu Kristo kuwaita watu na kuanza kuwahubiria katika Galilaya,aliwaita wavuvi  hawa,Simon na ndugu yake,Andrea,kisha akawaita Yakobo na ndugu yake,Yohana.Yesu Kristo aliwaita hawa watu ili kuwa wanafunzi wake, ambapo walitakiwa kujifunza vyema Neno kisha waje kupewa kazi kama mitume.Ndugu zangu katika Kristo imekuwa mara nyingi sana tunaposoma vitabu vya watumishi mbali mbali hatuangalii maneno yenye utashi wa kiroho na ukimbilia yale yenye utashi wa kimwili,Wanadamu leo tunasema tunamtegemea Mungu,tunasema tunamtanguliza Mungu ila siyo kivitendo bali tunayosema yote yanaishia hewani ,hewani kivipi!yanii kimaneno na siyo kivitendo.Nasema hivi kwa maaana kwamba Yesu Kristo ndiye aliyewachagua watu wale;siyo wao waliojichagua wala siyo wao waliojichagulia kazi ile.Leo kila mmoja wetu anapo mahali pa kufanyia huduma lakini siyo wote waliokuwa radhi kumfuata Yesu kristo ili kumruhusu yeye kutuongoza na kuwa ndiye mwenye kutuchagulia sisi;
Mr. & Mrs. Nelson
-Huduma.
-Kazi.
-Biashara.
-Vipawa.
-Ndoa#mke/mume
-Katika kulitekeleza hili yani ukaitwa kama akina Simon na ndugu yake,Andrea ,kisha Yakobo na ndugu yake, Yohana ,fahamu kabisa utaitajika kupimwa kwa kupewa JARIBU; na jaribu hilo litakuwa la kiMungu kama alivosema Katibu Mkuu katika Neno alilo tuhubiria na utapewa Jaribu ambalo ukilishinda basi litakupa uhalali wa wewe kuwa;
-Muhudumu wa Kweli utakaye tumiwa vyema na Roho Mtakatifu ukihudumu katika Injili ya kweli ile ya Kristo.
-Kazi ya kweli itakayo kupatia muda wa kumtukuza nayo Mungu,itakupa kipato,itakupa maendeleo na itakuongeza utumishi wako katika Ufalme wa mbinguni.
-Biashara ya kweli kimwili na kiroho,yenye faida za kuonekana zenye kumrudishia Mungu shukrani.
-Vipawa sahihi vyenye ushuhuda wa kweli wa kumvua Mwanadamu yule asiye amini Ukuu wa Mungu katika Utatu Mtakatifu.
-Ndoa yenye Amani,Faraja na Upendo ule wa tunda la roho ulionenwa katika Kitabu cha Wakorintho na kujidhihirisha kwa Yesu Kristo pale msalabani.
-Kwenye maisha ya sasa tumekuwa tukiishi  kama wanadamu wenye shingo ngumu sana,mara nyingi utakuta tunaenda makanisani kama waumini lakini hatuoni ongezeko la imani zetu na hata tukitaka kuongezwa tunashindwa tukifika kiwango au tunaanguka kwenye Interview/Mtihani ambao tunajifunza hapa kama JARIBU,na kuishia kulalamika.Tunapokuwa chuo au tunapofanya biashara flani,ama kazi yo yote,na ukagundua vitu hivi haviongezeki  chukuwa hatua.Utaona ukianza vina ishia nusu,ukienda ukafika haviendelei vinakufa,utavianda na vitaonyesha mwanga mara giza.hatua hapa ni kurudi darasani ukajifunze kushinda MAJARIBU mbayo ndiyo MTAJI wa MAFANIKIO yako.Njia zimetasha tajwa sana.KUSHIKA NENO NA KULISHI/KUOMBA BILA KUKOMA.
-Biblia inatufunza juu ya haya kwenye habari ya kipindi cha Yesu Kristo,katika sinagogi moja ambalo Yesu kristo alikuwepo kumbe alikuwepo na kijana ambaye alikuwa amepagawa na pepo mchafu.Jambo la kushangaza ni kwamba Yesu Kristo hakukemea bali huyu pepo ndani ya huyo mtu akaanza kupiga kelele kwamba Yesu Kristo amuachie alivyo ndani ya maisha ya huyu Kijana.Pepo hili lilifanya hivyo maana lilishazoea kuishi na huyu Kijana na mbaya zaidi Biblia inatuambia huyu kijana alikuwa mshirika wa siku nyingi wa hilo sinagogi na bado ibada hizo za sinagogi hazikuweza muweka huru.
-Sikia mtu wa Mungu unaye soma hitimisho hili nikuhubirie,tizama umekuwa mkristo siku nyingi na una pepo;(pepo la tabia chafu kadha wa kadha zilizoonywa katika Torati,tizama uwovu wa aina nyingi uliotajwa kama kitu cha kuepukwa bado umekushika mfano wa pepo,shida na taabu za kutosha ulizopitia na unazopitia zimekaa kama pepo na kuridhika,umaskini kimwili na kiroho umekukaa kama pepo,hofu kiimani na kimtizamo imekaa nawe bila mabadiliko kama pepo,macho ya rohoni yasiyo na uwezo mzuri wa kumuona mumeo au mkeo,ubongo wa rohoni usio na ufahamu wa kutosha wa kutambua Baraka za Bwana,roho za visasi,vinyongo),haya kwenye mabano ni baadhi ya mifano inayofananishwa na yule pepo  iliye kuwa ndani ya kijana,kijana muhumini wa sinagogi.
~Sikia mwana wa Mungu leo hapa PLACE OF PEACE COMMUNITY tunakuambia kaa tayari maana Yesu Kristo yuko hapa kukueka huru,huna haja ya kuangaika,wewe jitahidi kutulia kwa Mungu,shika unayofunzwa hapa na jitahidi kufanyia kazi na utaona tuu hayo yaliyofananishwa na pepo wa kijana wa sinagogi yataenda kufunguliwa.Leo kupitia nguvu ile Yesu Kristo aliyokuwa nayo pale sinagogi,nakuambia hilo pepo halina HAKI ya kuishi ndani yako,na Yesu kristo leo anakwenda kuviamuru vikutoke,AMENI.

-Nikuache na ‘’home work’’Je,watu wanasikia habari za Yesu Kristo kutoka kwetu wakati sisi tunapokwenda ofisini?biasharani?chuoni?mashuleni?mtaani?au majumbani mwetu pindi tukitoka kwenye sehemu Injili ya Kweli yaani habari za maisha ya Yesu Kristo,Injili ya kweli ya Ukuu wa jina la Mungu!Injili ya kweli ya Ahadi za Mungu kwa Wanadamu! Agano la Mungu kwa wanadamu!na mahubiri hayo unapata,Heman,Semina, au Makanisani?.#Barikiwa sana Mwana wa Mungu uliye fanikiwa kusoma hadi mwisho na ukatunzwe na neno hili ukisaidiwa na Roho Mtakatifu kulifanya likawe kweli yani likawe ni sehemu ya maisha yako(LIFESTYLE).

0 comments :

Somo la leo 11/09/2015

Bwana Yesu Asifiwe wapendwa


Tuombe.
 Bwana Yesu tunasema asante sana kwa wiki hii nzima ambapo ulikuwa pamoja nasi tangu mwanzo mwa wiki mpaka siku hii ya Ijumaa. Ulikuwa pamoja nasi katika semina yetu yenye kichwa " Jinsi ya kushinda majaribu kiroho na kimwili". Asante kwa maneno mbalimbali yaliyohubiriwa. Pia naomba ukawe pamoja nasi kwa siku ya leo ambapo tunaenda kumalizia semina hii. Ukatupe Roho wako Mtakatifu ili Atuwezeshe kuelewa yote tunayopaswa kuyafahamu kwa Utukufu wa Jina Lako. Amen!

Neno la asubuhi ya leo linatoka ktk kitabu cha Luka 4:1-9. Nitasoma mistari minne ya Kwanza kama ifuatavyo:
Mr Atupele Mwakalinga
1-      Kisha Yesu, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akarudi kutoka Yordani akaongozwa hadi jangwani. Alikaa huko jangwani siku arobaini. 2-akijaribiwa na shetani. Siku zote hizo hakula cho chote , kwa hiyo baada ya muda huo aliona njaa.3-Shetani akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate.”4-Yesu akamjibu, “Imeandikwa katika maandiko, ‘mtu haishi kwa chakula tu.’

Neno tajwa hapo juu na sana kama utasoma mistari yote, linatuonyesha jinsi Yesu alivyoshinda majaribu. Neno linatuambia kabla ya kujaribiwa Yesu alikuwa amejaa Roho Mtakatifu, hivyo kwa maana nyingine ni kwamba Roho Mtakatifu, huongoza kushinda majaribu kama tutakuwa naye kwa wingi katika mioyo yetu.
 Pia tunajifunza kuwa kwa kila jaribu, Yesu alikuwa analishinda kwa kifungu cha neno katika Biblia, alikuwa anasema “imeandikwa....". Hivyo basi ili kushinda majaribu ni lazima neno la Mungu likae kwa wingi ndani mwetu.
 Pia Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa "kesheni msije mkaingia majaribuni"...hili pia linatukumbusha kusali mara kwa mara ili tusije kuingia majaribuni.
 Sala ya Baba Yetu Uliye mbinguni....., inasema pia..." usitutie kwenye majaribu...” Hivyo ni vyema kumwomba Mungu atuepushe na majaribu. Lakini tukumbuke pia wakati mwingine, Mungu hukubali majariibu yatupate lakini tukiendelea kumtumaini yeye atatupa mlango wa kutokea.

Naomba Bwana Yesu azidi kuwabariki Ijumaa hii ya leo, mnapokwenda kulitafakari neno hili la leo. Amina.


2 comments :

Somo la leo 10/09/2015

Shaloom wana wa Mungu  katika Hemani mwa Mahali pa Amani

Ni asubuhi njema napenda kumbariki  Mungu wetu kwa kunipa hii nafasi ya kusema nawe juu ya habari njema ya Injili ya kweli kupitia semina hii yenye kichwa  cha somo kisemacho
#Jinsi ya Kushinda Majaribu Kiroho/Kimwili #
 ~Tumekuwa na wahudumu kila siku na tumekuwa tukipata kujifunza mengi kwa kila mmoja alivoguswa na Roho wa Bwana.Asubuhii hii tunaendelea na semina yetu,na leo nataka tukajifunze jinsi mwanadamu anpo fikia kumjaribu Mungu.Maana hatujifunzi sisi tu kama wanadamu kushinda majaribu lakini pia sisi kama wanadamu kushinda majaribu kwa kumjaribu Mungu.Utaweza jiuliza inakuwaje mimi kumjaribu Mungu lakini fahamu Yesu Kristo alimwambia Shetani  imeandikwa’’usimjaribu Bwana Mungu wako’’hii ikidhirisha ata sisi wanadamu tunamjaribu mara nyingi Bwana Mungu wetu.Tutaenda kusoma Neno la leo na tutalipata katika Kitabu cha KUTOKA,
**Kutoka17:2 kwa hiyo hao watu wakateta na Musa,wakasema,Tupe maji tunywe.Musa akawaambia,kwani kuteta na mimi?Mbona mnamjaribu BWANA?
Na Mr. Nelson
~Yesu Kristo wakati wote alikuwa anafikiria kuhusu mtu kamili na haja zake zote-sio mwili na magonjwa yake tu,bali roho na nafasi vile vile.Kazi yake ya kufundisha,kuokoa,na kuponya zote zilikwenda pamoja.Si kitu kinachowezekana kuondoa huduma ya uponyaji kutoka katika huduma ya kuokoa.Hizo zote zilikuwa ni kwa ajili kusudi moja tu-kuwageuza watu kutoka dhambini,kumwelekea Mungu.Utaweza shangaa inakuwaje Neno linamuongelea Musa nami nina anza na habari za Yesu Kristo!Nia yangu nataka upate picha hizi mbili.Kwanza kabisa Musa alikuwa na wana wa Israel jangwani na walikuwa wakipitia magumu na magumu hayo yalikuwa juu ya wao kukombolewa toka katika utumwa wenye mateso toka Misri kisha kuponywa na mateso ya Misri.Katika kuongozwa na ukombozi wa Musa utaona utofauti na ukombozi wa Yesu Kristo kwa wanadamu.

~Ukisoma Neno utagundua kitu hapa kwamba  wana wa Israel walipatwa na kiu na nia ya Mungu kufanya yote kwao ni ili wao waanze kumtegemea yeye na siyo mwanadamu ,Mungu alitaka wakafahamu kabisa kwamba yeye ndiye Mungu wa kweli yeye awezaye yote na siyo mwanadamu.Wanadamu wengi wanapoingia kwenye mahusiano ya kimapenzi lazima kila mmoja atahitaji nafasi ya kuzihirisha penzi lake la kweli kwa mwenza wake,na  katika zoezi hili kuna wale ufikia mahali wakaelewa na kuna wale uchukulia hali hizo za kuonyeshana ukweli wa penzi walilobeba ni la kweli .Wengine hali hii kuna atakaye ichukuwa kama vile mwenza wake ni "mpenzi bwege" au "buzi flan"na uwa itamuumiza mtu anaye jitoa pale atakapofahamu unachukuliwa ndivyo sivyo,hali hii ya kujizihirisha uja kwa vile mmoja wa wenza hao ataitaji mwenza wake afahamu anapendwa na asiangalie tena wengine bali yeye tuu.
~Tukirudi kwenye neno utajifunza kuwa Musa anawaambia...mbona mnamjaribu BWANA?unafikiri ni mara ngapi katika maisha yako umemjaribu Bwana..!!Je umewezaje kushinda Jaribu hilo?.
Mara ngapi wewe kama mwanadamu umemjaribu BWANA?? na ahadi zako labda akikupa mume/mke utamtumaini na kumtukuza sana Mungu?
Mara ngapi wewe kama mwanadamu umemjaribu BWANA kumwambia ukikupa kazi utamtolea muda wako kwa mambo yake na sadaka nzuri?
Mara ngapi wewe kama mwanadamu umemjaribu BWANA? kwa kumwambia nipe gari siwezi kwenda semina,kanisan mkesha,kanisan ibada ya alfajiri na alipokupa unalitumia sivyo?
Mara ngapi wewe kama mwanadamu umemjaribu BWANA kwa kumwambia nataka extra cash ndiyo nisiibe tena kazini nab ado waiba kwa kuongeza hesabu au kupunguza hesabu ama kugushi risiti mbalimbali?
Mara ngapi wewe kama mwanadamu umemjaribu BWANA ukisema sitaki tena wanaume/wanawake hakuna mwaminifu uku ukisema Mungu alishakuumbia mke au mume mwema?
Mara ngapi wewe kama mwanadamu unamjaribu BWANA kwa kumuomba mchumba na kabla hajakujibu  akuletee unaanza kutumia rafiki zako wa kike na kiume wakupatie mchumba,umeanza kutumia fedha zako au nafasi yako kazini au uwezo wako kibiashara?.
Ndugu katika Kristo fahamu maisha yako unayopitia leo ni maisha ya wana wa Israel na usije kumjaribu BWANA kwa kuomba kitu kwa Mtu kisa amechelewa kukupa au kisa umefika mahali changamoto zimezidi,fahamu yeye atakupa kwakuwa alishasema ukimtumikia atakuwa nawe popote na kwa hali yoyote, amekuokoa ili akuongoze. Acha kulalamika kwa watu,acha kunung'unika kwa watu ukisema “hivi BWANA yu kati yetu au sivyo”,endelea kumnyenyekee na kumtii zaidi hasa kwenye wakati uwo mgumu nah ii ndio njia ya kushinda jaribu lako ulilo mjaribu Mungu.Utashinda jaribu lako kwa kumrudishia ahadi zake na sio kumrudishia uliyo wahi pitia kwa shida,taabu na mateso mengi ukimwambia hayo yalikuwa mazuri zaidi ya unayokumbana nayo.Anasema katika neno lake kwamba “shukuruni kwa kila jambo”hii ina maana kwamba changamoto,shida na tabu unazopitia ushukuru kwakuwa ukizimaliza mpendwa utaenda kupokea kitu chema sana kwenye Ayubu anakifananisha na dhahabu.Tunakushukuru kwa maana ametusikia,ametuletea changamoto,tabu na shida hizo ili tukizipitia tutapata tulichoandaliwa.Ndugu yangu yawezekana hujashika vizuri hapa,nataka ufahamu kwamba Mungu upend asana atukuzwe katika maisha yetu,hivo unapoomba kitu ndio nafasi yake ya kutukuzwa na ndio maana ukupitisha katika eneo la kuthaminisha utayari wako wa kupokea ulichoomba lakini kwake pia kikaonekana kwa wengine ili wakamtukuze.


Hivyo basi tufahamu kwamba matokeo ya changamoto,shida na tabu tunazokumbana nazo hasa pale tumeshamshirikisha Mungu tunaitaji kutambua ameshatusikia tulichoomba na tuko katika hali ya kuandaliwa kuja kupokea rasmi kile tumeomba.Barikiwa sana na Mungu ukiongezwa na Roho wa Mungu katika kulielewa vyema somo hili.Amen.

0 comments :

Somo la Leo 09/09/2015

Shaloom  Wana wa Mungu. Nawasalimu nyote Katika Jina la Yesu

Namshukuru Mungu kwa asubuhi njema ni matarajio yangu ninyi nyote mmeamshwa vyema katika uzima wake.Basi ni wasaa mwengine mzuri wa siku hii ya Jumanne tukiendelea na semina yetu yenye kichwa kisemacho#Jinsi ya kushinda majaribu kiroho/Kimwili kama Mwanadamu#.Kaka Mugabe jana alifungua semina yetu na alitueleza msingi wa haswa wa wapi Jaribu linatoka na akatupa namna mojawapo ya kushinda akisema kwa habari ya kushika Neno la Mungu,jioni Dada Irene akaeka msingi nay eye akamtumia  Ayubu na kutoa tahadhari kwamba sio lazima Jaribu litoke kwa Mtu mbaya bali ata mtu wa karibu sana nawe ataweza kufanyika Jaribu.
Na Mr. Nelson...Mratibu
~Leo nataka tukatizame upande mwengine wa Jaribu na kabla sijaingia kwenye Neno ntapenda nirudi kwenye neno la jana toka kwa Kaka Mugabe,kuhusu kipindi Yesu Kristo anajaribiwa na Shetani.Shetani ni mjanja sana na mwenye mbinu nyingi.Kwanza kabisa yeye alijaribu kumwambia Yesu Kristo kwamba Bwana alikuwa na kila haki ya kuyageuza mawe kuwa mkate kwa sababu Yesu Kristo kweli alikuwa Mwana wa Mungu.Maneno yale"Ukiwa ni Mwana wa Mungu,"hayana maana ya kwamba Shetani alikuwa na mashaka na Yesu Kristo kwamba hakuwa Mwana wa Mungu.Maneno haya kweli  yanamaanisha kwamba‘Kwa vile wewe ni Mwana wa Mungu,’au "Kwa sababu wewe ni Mwana wa Mungu".Jaribu hapa lilikuwa wapi?Lilikuwa katika Shetani kujaribu kumfanya Yesu Kristo kuyageuza mawe yale kuwa mkate kwa ajili ya faida yake tu,ili kujipendeza mwenyewe.
~Tuingie kwenye Neno letu la leo na tukasome  kitabu cha,#Wamuzi 7:4 BWANA akamwambia Gideoni; Hata sasa watu hawa ni wengi mno; uwalete chini majini, nami nitawajaribu huko kwa ajili yako; kisha itakuwa ya kwamba yule nitakayekuambia, Huyu atakwenda pamoja nawe, ndiye atakayekwenda pamoja nawe; na mtu yule nitakayekuambia, Huyu hatakwenda pamoja nawe, basi mtu huyo hatakwenda.
~Kama nilivoanza na utangulizi tunagundua Shetan ametumia majaribu kwa faida yake na majaribu yakawa faida ya Kristo pia.Hapa tunasoma habari za Gideoni ambaye alikuwa mtumishi mzuri sana wa Mungu tena yule aliyekuwa akiitisha mahitaji kwa maombi ya vitendo.Mara nyingi sana kama wanadamu tumekuwa tukisikia watu wakichukulia Majaribu kama Mikosi,Laana,shida za dunia au dhambi flani.Bila kusahau majaribu yana pande mbili:
1-Upande wa Mungu kama kipimo cha mcha Mungu na Imani yenye utayari.
2-Upande wa shetani kama njia ya kukupotesha usahihi wa kufikia Mbaraka wako na kuangukia kwenye Uovu.
~Ukisoma Biblia utafahamu Gideoni aliteuliwa na Mungu, akiwa ni mtoto mdogo wa Yoashi. Mungu akamteuwa ili kwenda kuwaokoa wana wa Israel uko MIDIANI.Na ndipo alipomuitisha Mungu mambo kadha kupata uwakika wa yale anataka kufahamu toka kwa Mungu.Katika Neno hili mwana wa Mungu tunasoma Gideoni anapewa ahadi na Mungu katika kupatiwa watu sahihi ,hii ilimaanisha Gideoni hakuwa ametambua vyema kwa kiasi cha  uwezo wa hekima watu sahihi wa kuongozana nae katika ukombozi na ndio maana  akaitaji uwakika kwa Mungu.Hii ata leo ipo hapa duniani,sisi kama wanadamu bado hatuna uwakika wa kumsemea mtu kama mtu kamili ila Mungu kwa uwezo wake na kwakuwa yeye ndio muumbaji wetu basi atakuwa ndio 100% kutupa uwakika wa mwanadamu sahihi kwa jambo sahihi.
~Ndugu zangu wana pP,neno hapa linazungumzia Jaribu toka kwa Mungu ili kutoa jibu sahihi na kupata watu sahihi,Jaribu la Mungu katika Neno hili linaweza kuja kwako leo na hata sisi hapa Katika Jumuiya ya Mahali pa Amani (pPc)na ata kwako msomaji katika wengi flani mliyojikusanya ili kufanya huduma litakuja.Tuko wengi hapa na tunaonyesha ule uhitaji wa kutii kiu ya kumjua Mungu na kutumiwa kama Ishara au Alama za mambo yake na Wana wa Ufalme wake,bali lazima tuta pimwa kwa kujaribiwa,sijajua jaribu litakuwaje ila lazima tutapimwa na wale tutakuwa tumepita basi hao ndio haswa tutaendelea na Jumuiya.Sikutishi ila nakuekea msingi kwa maana Mungu wetu anafahamu uhitaji wa Huduma yake na anafahamu fika  nani na nani wanaitaji kufanywa sehemu ya huduma zake na wangapi wako tayari kuona Mungu anatokea katika maisha yao, hivyo  tujitahidi sana kujifunza kwani kunafaida kubwa na nzuri ukihakikiwa na Mungu kumtumikia.Basi kwa sasa nikuache na Tafakari hii na Roho wa Mungu atuguse tutaenda kujifunza zaidi kupitia neno hili juu ya sisi kuitisha  jaribu katika kupata uwakika kwa Mungu.Barikiwa sana.

3 comments :