Shaloom Wana wa
Mungu. Nawasalimu nyote Katika Jina la Yesu
Namshukuru Mungu kwa
asubuhi njema ni matarajio yangu ninyi nyote mmeamshwa vyema katika uzima
wake.Basi ni wasaa mwengine mzuri wa siku hii ya Jumanne tukiendelea na semina
yetu yenye kichwa kisemacho#Jinsi ya
kushinda majaribu kiroho/Kimwili kama Mwanadamu#.Kaka Mugabe jana alifungua
semina yetu na alitueleza msingi wa haswa wa wapi Jaribu linatoka na akatupa
namna mojawapo ya kushinda akisema kwa habari ya kushika Neno la Mungu,jioni
Dada Irene akaeka msingi nay eye akamtumia
Ayubu na kutoa tahadhari kwamba sio lazima Jaribu litoke kwa Mtu mbaya
bali ata mtu wa karibu sana nawe ataweza kufanyika Jaribu.
![]() |
Na Mr. Nelson...Mratibu |
~Tuingie kwenye Neno
letu la leo na tukasome kitabu cha,#Wamuzi 7:4 BWANA akamwambia Gideoni; Hata
sasa watu hawa ni wengi mno; uwalete chini majini, nami nitawajaribu huko kwa
ajili yako; kisha itakuwa ya kwamba yule nitakayekuambia, Huyu atakwenda pamoja
nawe, ndiye atakayekwenda pamoja nawe; na mtu yule nitakayekuambia, Huyu
hatakwenda pamoja nawe, basi mtu huyo hatakwenda.
~Kama nilivoanza na
utangulizi tunagundua Shetan ametumia majaribu kwa faida yake na majaribu
yakawa faida ya Kristo pia.Hapa tunasoma habari za Gideoni ambaye alikuwa
mtumishi mzuri sana wa Mungu tena yule aliyekuwa akiitisha mahitaji kwa maombi
ya vitendo.Mara nyingi sana kama wanadamu tumekuwa tukisikia watu wakichukulia
Majaribu kama Mikosi,Laana,shida za dunia au dhambi flani.Bila kusahau majaribu
yana pande mbili:
1-Upande wa Mungu
kama kipimo cha mcha Mungu na Imani yenye utayari.
2-Upande wa shetani
kama njia ya kukupotesha usahihi wa kufikia Mbaraka wako na kuangukia kwenye
Uovu.
~Ukisoma Biblia
utafahamu Gideoni aliteuliwa na Mungu, akiwa ni mtoto mdogo wa Yoashi. Mungu akamteuwa ili kwenda
kuwaokoa wana wa Israel uko MIDIANI.Na ndipo alipomuitisha Mungu
mambo kadha kupata uwakika wa yale anataka kufahamu toka kwa Mungu.Katika Neno
hili mwana wa Mungu tunasoma Gideoni anapewa ahadi na Mungu katika
kupatiwa watu sahihi ,hii ilimaanisha Gideoni hakuwa ametambua vyema kwa kiasi
cha uwezo wa hekima watu sahihi wa
kuongozana nae katika ukombozi na ndio maana akaitaji uwakika kwa Mungu.Hii ata leo ipo
hapa duniani,sisi kama wanadamu bado hatuna uwakika wa kumsemea mtu kama mtu
kamili ila Mungu kwa uwezo wake na kwakuwa yeye ndio muumbaji wetu basi atakuwa
ndio 100% kutupa uwakika wa mwanadamu sahihi kwa jambo sahihi.
~Ndugu zangu wana
pP,neno hapa linazungumzia Jaribu
toka kwa Mungu ili kutoa jibu sahihi na kupata watu sahihi,Jaribu la Mungu
katika Neno hili linaweza kuja kwako leo na hata sisi hapa Katika Jumuiya ya
Mahali pa Amani (pPc)na ata kwako msomaji katika wengi flani mliyojikusanya ili
kufanya huduma litakuja.Tuko wengi hapa na tunaonyesha ule uhitaji wa kutii kiu
ya kumjua Mungu na kutumiwa kama Ishara au Alama za mambo yake na Wana wa
Ufalme wake,bali lazima tuta pimwa kwa kujaribiwa,sijajua jaribu litakuwaje ila lazima tutapimwa na wale tutakuwa tumepita
basi hao ndio haswa tutaendelea na Jumuiya.Sikutishi ila nakuekea msingi kwa
maana Mungu wetu anafahamu uhitaji wa Huduma yake na anafahamu fika nani na nani wanaitaji kufanywa sehemu ya
huduma zake na wangapi wako tayari kuona Mungu anatokea katika maisha yao,
hivyo tujitahidi sana kujifunza kwani
kunafaida kubwa na nzuri ukihakikiwa na Mungu kumtumikia.Basi kwa sasa nikuache
na Tafakari hii na Roho wa Mungu atuguse tutaenda kujifunza zaidi kupitia neno
hili juu ya sisi kuitisha jaribu katika kupata uwakika kwa
Mungu.Barikiwa sana.
barikiwa sana kwa neon zuri sana mtumishi.
ReplyDeletenimedaka vitu hapo
Amen
DeleteNeno zuri Ubarikiwe
ReplyDelete