Shaloom wana wa Mungu
katika Hemani mwa Mahali pa Amani
Ni
asubuhi njema napenda kumbariki Mungu
wetu kwa kunipa hii nafasi ya kusema nawe juu ya habari njema ya Injili ya
kweli kupitia semina hii yenye kichwa
cha somo kisemacho
#Jinsi ya Kushinda Majaribu
Kiroho/Kimwili #
~Tumekuwa na wahudumu kila siku na tumekuwa
tukipata kujifunza mengi kwa kila mmoja alivoguswa na Roho wa Bwana.Asubuhii hii tunaendelea na semina
yetu,na leo nataka tukajifunze jinsi mwanadamu anpo fikia kumjaribu Mungu.Maana
hatujifunzi sisi tu kama wanadamu kushinda majaribu lakini pia sisi kama
wanadamu kushinda majaribu kwa kumjaribu Mungu.Utaweza jiuliza inakuwaje mimi
kumjaribu Mungu lakini fahamu Yesu Kristo alimwambia Shetani imeandikwa’’usimjaribu Bwana Mungu wako’’hii ikidhirisha
ata sisi wanadamu tunamjaribu mara nyingi Bwana Mungu wetu.Tutaenda kusoma Neno
la leo na tutalipata katika Kitabu cha KUTOKA,
**Kutoka17:2 kwa hiyo hao
watu wakateta na Musa,wakasema,Tupe maji tunywe.Musa akawaambia,kwani kuteta na
mimi?Mbona mnamjaribu BWANA?
![]() |
Na Mr. Nelson |
~Yesu
Kristo wakati wote alikuwa anafikiria kuhusu mtu kamili na haja zake zote-sio
mwili na magonjwa yake tu,bali roho na nafasi vile vile.Kazi yake ya
kufundisha,kuokoa,na kuponya zote zilikwenda pamoja.Si kitu kinachowezekana
kuondoa huduma ya uponyaji kutoka katika huduma ya kuokoa.Hizo zote zilikuwa ni
kwa ajili kusudi moja tu-kuwageuza watu kutoka dhambini,kumwelekea
Mungu.Utaweza shangaa inakuwaje Neno linamuongelea Musa nami nina anza na
habari za Yesu Kristo!Nia yangu nataka upate picha hizi mbili.Kwanza kabisa
Musa alikuwa na wana wa Israel jangwani na walikuwa wakipitia magumu na magumu
hayo yalikuwa juu ya wao kukombolewa toka katika utumwa wenye mateso toka Misri
kisha kuponywa na mateso ya Misri.Katika kuongozwa na ukombozi wa Musa utaona
utofauti na ukombozi wa Yesu Kristo kwa wanadamu.
~Ukisoma
Neno utagundua kitu hapa kwamba wana wa
Israel walipatwa na kiu na nia ya Mungu kufanya yote kwao ni ili wao waanze
kumtegemea yeye na siyo mwanadamu ,Mungu alitaka wakafahamu kabisa kwamba yeye
ndiye Mungu wa kweli yeye awezaye yote na siyo mwanadamu.Wanadamu wengi
wanapoingia kwenye mahusiano ya kimapenzi lazima kila mmoja atahitaji nafasi ya
kuzihirisha penzi lake la kweli kwa mwenza wake,na katika zoezi hili kuna wale ufikia mahali
wakaelewa na kuna wale uchukulia hali hizo za kuonyeshana ukweli wa penzi
walilobeba ni la kweli .Wengine hali hii kuna atakaye ichukuwa kama vile mwenza
wake ni "mpenzi bwege" au "buzi flan"na uwa itamuumiza mtu
anaye jitoa pale atakapofahamu unachukuliwa ndivyo sivyo,hali hii ya
kujizihirisha uja kwa vile mmoja wa wenza hao ataitaji mwenza wake afahamu
anapendwa na asiangalie tena wengine bali yeye tuu.
~Tukirudi
kwenye neno utajifunza kuwa Musa anawaambia...mbona mnamjaribu BWANA?unafikiri
ni mara ngapi katika maisha yako umemjaribu Bwana..!!Je umewezaje kushinda
Jaribu hilo?.
Mara
ngapi wewe kama mwanadamu umemjaribu BWANA?? na ahadi zako labda akikupa
mume/mke utamtumaini na kumtukuza sana Mungu?
Mara
ngapi wewe kama mwanadamu umemjaribu BWANA kumwambia ukikupa kazi utamtolea
muda wako kwa mambo yake na sadaka nzuri?
Mara
ngapi wewe kama mwanadamu umemjaribu BWANA? kwa kumwambia nipe gari siwezi
kwenda semina,kanisan mkesha,kanisan ibada ya alfajiri na alipokupa unalitumia
sivyo?
Mara
ngapi wewe kama mwanadamu umemjaribu BWANA kwa kumwambia nataka extra cash ndiyo
nisiibe tena kazini nab ado waiba kwa kuongeza hesabu au kupunguza hesabu ama
kugushi risiti mbalimbali?
Mara
ngapi wewe kama mwanadamu umemjaribu BWANA ukisema sitaki tena wanaume/wanawake
hakuna mwaminifu uku ukisema Mungu alishakuumbia mke au mume mwema?
Mara
ngapi wewe kama mwanadamu unamjaribu BWANA kwa kumuomba mchumba na kabla
hajakujibu akuletee unaanza kutumia
rafiki zako wa kike na kiume wakupatie mchumba,umeanza kutumia fedha zako au
nafasi yako kazini au uwezo wako kibiashara?.
Ndugu
katika Kristo fahamu maisha yako unayopitia leo ni maisha ya wana wa Israel na
usije kumjaribu BWANA kwa kuomba kitu kwa Mtu kisa amechelewa kukupa au kisa
umefika mahali changamoto zimezidi,fahamu yeye atakupa kwakuwa alishasema
ukimtumikia atakuwa nawe popote na kwa hali yoyote, amekuokoa ili akuongoze.
Acha kulalamika kwa watu,acha kunung'unika kwa watu ukisema “hivi BWANA yu kati
yetu au sivyo”,endelea kumnyenyekee na kumtii zaidi hasa kwenye wakati uwo
mgumu nah ii ndio njia ya kushinda jaribu lako ulilo mjaribu Mungu.Utashinda
jaribu lako kwa kumrudishia ahadi zake na sio kumrudishia uliyo wahi pitia kwa
shida,taabu na mateso mengi ukimwambia hayo yalikuwa mazuri zaidi ya
unayokumbana nayo.Anasema katika neno lake kwamba “shukuruni kwa kila jambo”hii
ina maana kwamba changamoto,shida na tabu unazopitia ushukuru kwakuwa
ukizimaliza mpendwa utaenda kupokea kitu chema sana kwenye Ayubu anakifananisha
na dhahabu.Tunakushukuru kwa maana ametusikia,ametuletea changamoto,tabu na
shida hizo ili tukizipitia tutapata tulichoandaliwa.Ndugu yangu yawezekana
hujashika vizuri hapa,nataka ufahamu kwamba Mungu upend asana atukuzwe katika
maisha yetu,hivo unapoomba kitu ndio nafasi yake ya kutukuzwa na ndio maana ukupitisha
katika eneo la kuthaminisha utayari wako wa kupokea ulichoomba lakini kwake pia
kikaonekana kwa wengine ili wakamtukuze.
Hivyo
basi tufahamu kwamba matokeo ya changamoto,shida na tabu tunazokumbana nazo
hasa pale tumeshamshirikisha Mungu tunaitaji kutambua ameshatusikia tulichoomba
na tuko katika hali ya kuandaliwa kuja kupokea rasmi kile tumeomba.Barikiwa
sana na Mungu ukiongezwa na Roho wa Mungu katika kulielewa vyema somo
hili.Amen.
0 comments :